Makosa Kwenye Mtandao Taratibu za Kufuata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makosa Kwenye Mtandao Taratibu za Kufuata

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Aug 24, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na watu kadhaa wanaulizia usalama wao pindi wanapojiunga na mitandao Fulani kwa katika kutoa maoni na kuweka michango yao mbalimbali wakiwa kwenye majukwaa hayo naomba nielezee taratibu ambazo zinaweza kuchukuliwa na watu haswa vyombo vya usalama endapo itaonekana mtu au kikundi hicho cha watu kinasababisha matatizo kwenye jamii zingine .


  Matatizo ninayozungumzia ni kama Kusambaza Picha za watu bila idhini yao , kazi za sanaa , Kutukana , Uwongo au kusambaza propaganda za chuki dhidi ya kundi Fulani la watu , Wizi kwa njia ya Mtandao , Kupanga Mipango ya kihalifu kwa njia ya Mtandao na mengine mengi ambayo yanaweza kuvunja amani ya sehemu Fulani , uaminifu au kutishia chuki na uadui kati ya makundi Fulani ya kijamii .


  Sasa hizi hapa chini ndio taratibu zinazofuatwa sehemu nyingi ambapo mambo kama haya yanatokea au kutokea lakini hii mara nyingi haihusiani na wale wenye blogu ambao wanaandika maoni yao wao binafsi au makundi ambayo yanatovuti zao binafsi ambazo wao wameshaandika malengo yao hii inahusiana zaidi na majukwaa wengi huita Forums ambapo watu hujiunga kwa ajili ya kutoa maoni , habari na masuala mengine ya kimaisha .


  HATUA ZINAZOCHUKULIWA
  1 - Mtu / Kampuni ataenda Kushitaki kwenye vyombo husika .

  2 - Mahakama pamoja na jeshi la polisi kwa kutumia sheria za nchi husika litawasiliana na Uongozi wa Forum au Jukwaa Husika kwa ajili ya kupatiwa Taarifa za Mhusika Huyo .
  Taarifa za Mtandao pamoja na mawasiliano yao huweza kupatikana kwa kutumia tovuti kama www.whois.ws unaweza kuingiza jina la tovuti na kupata mawasiliano ya jina la tovuti hiyo na mawasiliano mengine kisha utaweza kuwasiliana nao .

  3 – Taarifa zako zikipatikana watawasiliana na ISP ( Mtoa huduma Za Internet ) wako kwa ajili ya kujua wewe pamoja na Kuwasiliana na Mtandao unaotoa huduma za email zako kama zile yahoo au hotmail ingawa hii ni kwa asilimia 1 kati ya Mia hao Yahoo au hotmail wajibu maombi , kama domain yako imesahilwa kama unatumia kwa mfano wewe@maishabora.com hiyo inatumika hatua ya 2 Kuweza Kujua badala ya kuwasiliana na Yahoo moja kwa moja .

  4 – Kwa kuwa ISP wako ndio Mlinzi kati yako na mawasiliano ya Nje na kwa kuwa yeye ndio anakuwezesha kuwasiliana basi atatoa Taarifa hizi kwa vyombo hivyo kwa ajili ya uchunguzi na kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vingine vya sheria lakini hiyo pia inaweza kuwa ngumu kama nchi husika haina sheria ya masuala ya Mtandao au mawasiliano ya Electroniki na kama kampuni hizo za mawasiliano hazina sera ya kuhifadhi taarifa za wateja wao kwa kipindi Fulani .


  Nchi nyingi duniani kwa mfano zina sheria za kuhifadhi taarifa zote za mawasiliano kwenye nchi hiyo kuanzia simu za mikono mpaka matumizi ya barua pepe na tovuti na hizo haziwezi kufungwa moja kwa moja ikifungwa inakaa kwa siku 90 mpaka hapo itakapodhibitika kwamba hamna kosa lolote limetendeka kutumia anuani hiyo , masuala ya kodi na takwimu zingine za serikali .


  Naomba kuishia hapa Taratibu hizi zinaweza kubadilika kutokana na mazingira ya Maeneo ambayo Kosa limefanyika na aina la kosa hilo na kulingana na sheria za nchi au sehemu husika kuna baadhi ya maeneo kuonyesha picha za watu si kosa lakini mengine ni makosa kama baadhi ya nchi , nchi zingine kuonyesha picha za watoto wadogo ni kosa zingine sio kosa kwahiyo haya yote yanatakiwa kuzingatiwa .
  Yona F Maro
  www.ictpub.blogspot.com
   
Loading...