Makosa haya yana mchango mkubwa katika kuivunja ndoa!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,810
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,810 2,000
Kutokana na malezi au mazoea au pengine tabia zilizo katika mila na desturi zetu, tumejikuta mara nyingi tukiwafanyia wapenzi, waume au wake zetu tabia ambazo kutokana na mazoea hayo tunadhani au kuziita ‘vitu vidogo.’ Lakini kwa bahati mbaya katika huo udogo wake hutusababishia uhusiano wetu na wenzetu kwenda mrama.

Hebu tujiulize, inakuwaje pale tunapoona wenzetu wanafanya jambo ambalo kwa wakati kama huo halikupaswa kufanywa. Mara nyingi tunakuwa wakali au kuwalaumu na kudhani hiyo ndiyo njia bora. Kwa mfano mpenzi anasikiliza redio au kuangalia TV, badala ya kufanya kazi fulani muhimu ndani ya nyumba. Badala ya kutumia ujanja wa kiupendo kukataza jambo hilo, tunaweza kuwaambia, ‘inatosha bwana, hebu njoo huku ufanye kazi fulani…’ au ‘hebu zima hiyo TV, unaacha kazi fulani umeng’ang’ania TV tu’

Kwa upande wetu, kauli kama hii inaweza kuonekana kuwa kauli ndogo na ya kawaida sana na isiyo na madhara. Ukweli ni kwamba ina madhara kwa sababu siyo kauli ya upendo. Kauli au tendo lolote ambalo siyo la upendo huusogeza uhusiano kati ya watu wawili mbali zaidi siku hadi siku, ingawa tunaweza tusilione jambo hilo.

Pia ni vizuri wapenzi kujiepusha kutoa msaada pale ambapo hawajaombwa, hasa kwenye yale mambo au shughuli ambazo ni za kawaida ndani a nyumba. Jiko limekataa kuwaka, mwanamke anajaribu kulirekebsha ili liwake, wakati akifanya hivyo , mwanaume anajipeleka kimbelembele na kuanza kuomba apewe yeye kazi hiyo. Hili ni kosa, ingawa anayelifanya anadhani anafanya upendo.

Kwenye uhusiano inapendeza sana wapenzi kuachiana nafasi ya kujenga hali ya kujitegemea katika kusuluhisha au kutatua matatizo madogomadogo, hali ya kuachiwa mpenzi kujenga uhuru wa kutatua matatizo madogomadogo hufanya mpenzi kujiamini na kupata hisia za kuaminika. Wanaume ndio ambao hupenda sana kuingilia uhuru huu wa wanawake.

Kwa kawaida wanawake kabla hawajaomba msaada, huwa hawataki kusaidiwa katika kutatua matatizo haya. Ndio maana mara nyingi unasikia, ‘baba fulani, jiko lilikuwa limechafuka sana lakini nimelisafisha na sasa linawaka vizuri…’ hivi ndivyo wanawake wanavyotaka, kwani hapa hujenga hisia za kujiamini na kuaminika pia, hisia za kuweza na za kujitegemea.

 

Bucad

Senior Member
Joined
Aug 15, 2011
Messages
120
Points
0

Bucad

Senior Member
Joined Aug 15, 2011
120 0
Akhasante sana kwa tution ya bure nadhani ni somo tosha sana kwa wanaodhani mahusiano au ndoa ni kuishi na mtu tu!
 

Forum statistics

Threads 1,391,116
Members 528,369
Posts 34,074,053
Top