Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,713
Siku chache baada ya kutangaza kuridhika na mapendekezo ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kutompitisha kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye kinyanganyiro cha urais, Charles Makongoro Nyerere amejitosa kuwania ubunge katika Jimbo la Kawe, Dar es Salaam.
Pia, Profesa Sospeter Muhongo ambaye naye alikuwa miongoni mwa wagombea urais wa CCM, alichukua fomu ya kuwania Ubunge wa Musoma Vijijini. Baada ya kuchukua fomu, Waziri huyo wa zamani wa Nishati na Madini aliandika katika ukurasa wake wa Facebook: Leo nimechukua fomu nagombea ubunge wa Musoma Vijijini bado ninadhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania. Tusikate tamaa.
Aidha, aliyekuwa mgombea urais mwingine, Peter Nyalali amechukua fomu kuwania ubunge Jimbo la Mbagala, sanjari na Mwichumu Msomi na Dominic Francis Haule.
Baadhi ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Katibu wa Rais ni miongoni mwa waliojitokeza jana kuwania ubunge maeneo mbalimbali nchini.
Kawe: Mbali ya Makongoro, makada wengine 14 walijitokeza kuwania kiti hicho wakiwemo; Mtiti Butiku, Yusuph Nassoro, John Mayanja, Dickson Muze na Dk Wilson Babyebonela.
CHANZO: Mwananchi