Elections 2010 Makongolo mahanga aahidi kulifanya soko la buguruni kuwa la kimataifa

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Katika hali inayoonesha wagombea wa CCM kuishiwa sera na kuendekeza dhana ya kuwaona Watanzania ni mazuzu, mgombea wa Ubunge jimbo la Segerea Bw. Dr. Makaongolo Makanga ametoa ahadi kichekesho kwa wanachi wake baada ya kuwaahidi kuwa akichaguliwa atalifanya "soko la buguruni kuwa la kimataifa".

Mimi ninaishi jimbo la Segerea. Buguruni ni moja ya vitongoji vya jimbo hili ambavyo watu wamejenga kiholela na wengi ni masikini wa kipato. Huwezi kujenga Soko lenye hadhi ya Kimataifa mahala ambapo miundombinu ya ujenzi ni mibovu kama ilivyo Buguruni. Kama kuna kitongoji ambapo CCM inachukiwa kwa kiasi kikubwa na watu wana kiu ya mabadiliko, ni Buguruni. Ahadi ya Mahanga haina mashiko na inaweza kutafsiriwa kama kejeli.

Kwa miaka mitano ambayo Mahanga amekuwa mbunge amefanikiwa jambo moja tu:
Kujenga baa ya Nyantare maeneo ya Tabata Bima, ambayo hata hivyo inasemekana anaimilikki yeye.

  1. Ameshindwa kuunganisha Mawenzi na Kimanga kwa lami
  2. Ameshindwa kumalizia ujenzi wa kituo bora cha daladala Kimanga
  3. Ameshindwa japo kupunguza kero ya maji. Si ajabu Segerea kukosa maji mwezi mzima
  4. Lakini amejenga kumbi zake mbili za starehe kwa muda wa mwaka mmoja.

Hata hivyo, kila aliposema "ccm hoyee!!" waliojibu ni wale tu waliokuwa wamevalia matambala ya kupigia deki (vijifulana vya njano). Aliharibu zaidi alipoomba wananchi wamchague JK.

Source: NICHAGUE MIMI (ITV)
 
Kwanini hakulijenga wakati akiwa tayari ni mbunge kuanzia 2005 hadi mwaka jana? F.U.C.K HM
 
They are very desperate!! Dawa iko tu, 310/10/2010.:A S 112: tutawamwaga tu!!
 
aende zake kule maji huko segerea ni tatizo la kitaifa sasa. hakuna lolote la maana alilofanya.
 
Afadhali hata nyie huko kunatazamika, sisi huku alikotuacha uchafu mtupu!
 
nichague mimi (itv)-- kw nni unaiita hivo? Mahanga hayupo serious na halmashauri yake yote haipo serious wanaiba hela za wananchi. Watu wanakatwa kodi kwenye biashara zao hakuna mtu anayefanya biashara bure pale wote wanakatwa kodi pale lakini hamna kinachobadilika.
 
nichague mimi (itv)-- kw nni unaiita hivo? Mahanga hayupo serious na halmashauri yake yote haipo serious wanaiba hela za wananchi. Watu wanakatwa kodi kwenye biashara zao hakuna mtu anayefanya biashara bure pale wote wanakatwa kodi pale lakini hamna kinachobadilika.

NICHAGUE MIMI ni kipindi cha televisheni ya ITV ambapo wagombea hupewa muda wa kujinadi (nadhani wanalipia, si unajua Mengi ni Mchaga?).
 
katika hali inayoonesha wagombea wa ccm kuishiwa sera na kuendekeza dhana ya kuwaona watanzania ni mazuzu, mgombea wa ubunge jimbo la segerea bw. Dr. Makaongolo makanga ametoa ahadi kichekesho kwa wanachi wake baada ya kuwaahidi kuwa akichaguliwa atalifanya "soko la buguruni kuwa la kimataifa".

Mimi ninaishi jimbo la segerea. Buguruni ni moja ya vitongoji vya jimbo hili ambavyo watu wamejenga kiholela na wengi ni masikini wa kipato. Huwezi kujenga soko lenye hadhi ya kimataifa mahala ambapo miundombinu ya ujenzi ni mibovu kama ilivyo buguruni. Kama kuna kitongoji ambapo ccm inachukiwa kwa kiasi kikubwa na watu wana kiu ya mabadiliko, ni buguruni. Ahadi ya mahanga haina mashiko na inaweza kutafsiriwa kama kejeli.

Kwa miaka mitano ambayo mahanga amekuwa mbunge amefanikiwa jambo moja tu:
Kujenga baa ya nyantare maeneo ya tabata bima, ambayo hata hivyo inasemekana anaimilikki yeye.

  1. ameshindwa kuunganisha mawenzi na kimanga kwa lami
  2. ameshindwa kumalizia ujenzi wa kituo bora cha daladala kimanga
  3. ameshindwa japo kupunguza kero ya maji. Si ajabu segerea kukosa maji mwezi mzima
  4. lakini amejenga kumbi zake mbili za starehe kwa muda wa mwaka mmoja.

hata hivyo, kila aliposema "ccm hoyee!!" waliojibu ni wale tu waliokuwa wamevalia matambala ya kupigia deki (vijifulana vya njano). Aliharibu zaidi alipoomba wananchi wamchague jk.

Source: Nichague mimi (itv)

buguruni hiyo ni ile ambayo kila mwaka uongoza kwa kipindipindi kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya maji taka au nyingine? Huyo zuzu kweli.
 
Back
Top Bottom