Makonda: Wanaodai kuna tatizo la ajira, wana upungufu wa kufikiri!

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda, ameseme leo jijini Dar-es-salaam kuwa wale wanaopita na kudai kuna upungufu wa ajira, wao wenyewe ndio wana upungufu wa kufikiri.

Chanzo:Channel 10.
Makonda anatumika vibaya. Mwisho wa siku Hawa watu huwa wanaabika vibaya. Marekani wenyewe wenye uchumi mkubwa ambaye kila siku babake anapeleka bakuli kuomba wanatatizo la ajira. Sembuse yeye hapo Kndoni?
 
mimi nimemuelewa sn jamaa yuko makini,anatumia falsafa ya ukimwambia mtoto hana akili nae anajiona hana akili,kweli ajira zipo ila watz wenge wanataka ajira za kuzunguka kwenye kiti.
 
Makonda anatumika vibaya. Mwisho wa siku Hawa watu huwa wanaabika vibaya. Marekani wenyewe wenye uchumi mkubwa ambaye kila siku babake anapeleka bakuli kuomba wanatatizo la ajira. Sembuse yeye hapo Kndoni?
Imagine eti watu wa aina hii ndio watu wa kutuandikia katiba!!

Hakika ni shida!
 
hivi makonda ana umri gani? je ameoa? ana watoto? unaweza kuta unamdharau mtu kumbe bado anabalee make wanaobalehe ndo wanakuaga na mihemko.
 
Hivi huyu jamaa amesomea nini???nasikiaga ni mwanasheria...nitashangaa sana kama ikiwa kweli..
 
Enzi za Hayati JKN hiyo lugha ya hakuna ajira haikuwepo. Vijana waliokuwa wakizurura mitaa ya Kariakoo na Samora bila kuwa na shughuli maalum walikuwa wakisombwa na kupelekwa Gezaulole (enzi hizo likiwa pori lenye rutuba ya kufungua mashamba ya mihogo). Ninaweza kukubaliana na dogo Makonda kwamba huku vijijini ajira ni nyingi sana tunatafuta watu wa kuajiri na kujiajiri - kumbuka kilimo na ufugaji ndio uti wa mgongo wa uchumi. Inahitaji ka-ubunifu kadogo tu kutumia digrii ya UDSM au UDOM ukawa mjasiriamali katika agrobusiness. Ninaanza kukubali dogo Makonda una fikira pana pamoja na laana uliyobeba ya kumpa kichapo Mzee wetu Mzee Warioba.
 
Lowasa akichukuwa nchi,ndo atajua wasiokuwa na ajira wana upungufu wa akili kivipi,maana Lowasa akiwa Raisi Makonda ndo itakuwa kikomo cha huo ukuu wa wilaya

Mimi namuomba Mungu Lowassa awe ndo raisi wa TZ 2015, watu Kama Makonda, Nape... sijui watafisha haibu zao wapi katika nchi hi.
 
Ukiangalia utitiri wa watu wanaogombea urais kupitia CCM ndipo utajua kuwa kuna tatizo la ajira. Nafasi inayogombewa ni moja tu but angalia watu ambao tayari wameshaomba hiyo nafasi, na wengine bado wanaendelea. Ni sawa na zile ajira za uhamiaji. Uhitaji diploma kufikiria hilo.
 
Tatizo la ukosefu wa ajira nchini Tanzania ni kubwa kama ilivyo kwa nchi nyingine ulimwenguni. Kwa sasa ukosefu wa ajira Tanzania umefikia 11.7%. Naweza kusema asiyeona kama kuna tatizo la ukosefu wa ajira ana matatizo ya kufikiri.
 
kiboko yake lowasa .ngoja aingie amsweke segerea si alimwita fisadi ili apewe ukuu wa wilaya.tuunge mkono safari ya matumani
 
lowassa ni nyota angavu haiwezi kuzimwi ----- wa wagombea wanaotumwa kuja kumbana lowasa hawataweza.
 
Enzi za Hayati JKN hiyo lugha ya hakuna ajira haikuwepo. Vijana waliokuwa wakizurura mitaa ya Kariakoo na Samora bila kuwa na shughuli maalum walikuwa wakisombwa na kupelekwa Gezaulole (enzi hizo likiwa pori lenye rutuba ya kufungua mashamba ya mihogo). Ninaweza kukubaliana na dogo Makonda kwamba huku vijijini ajira ni nyingi sana tunatafuta watu wa kuajiri na kujiajiri - kumbuka kilimo na ufugaji ndio uti wa mgongo wa uchumi. Inahitaji ka-ubunifu kadogo tu kutumia digrii ya UDSM au UDOM ukawa mjasiriamali katika agrobusiness. Ninaanza kukubali dogo Makonda una fikira pana pamoja na laana uliyobeba ya kumpa kichapo Mzee wetu Mzee Warioba.

Wewe ha huyo dogo wako ndio muweke hako ka ubunifu ili hao mnaoona wana mawazo mafupi waanzie hapo kupata suluhisho. The HOW factor ndio inaumiza kichwa watu wengi. . . .. hao mnaoona wana mawazo mafupi! !!

Hebu tuwekee jinsi ya kuendesha hilo shamba la mihogo la hekari ishirini na mahitaji yake ili mtu apate wastani wa milioni moja tu kwa mwezi baada ya gharama zote utakuwa umesaidia wengi sana!!!!!
 
Back
Top Bottom