Makonda: Wakuu wa Wilaya waondoeni Machinga ndani ya siku 14

tunaelekea kwenye miaka hamsini ya uhuru
 
Wamerudi kwa kasi. Jana mchana kweupe nimekuta jamaa amewasha moto wa kuni katikati ya jiji pale Akiba, anapika bila wasiwasi kabisa! Oooh my country! Nikilinganisha na majiji walau niliyopitia kidogo kama Kuala Lumpur, naona aibu!
 
Inasemekana aliyeruhusu hali ya machinga kupanga bidhaa zao popote ni JPM. Ni hotuba aliyoitoa Mwanza. Hivyo kuzilaumu manispaa ni kuzionea hasa ukizingatia hazina vyombo vya dola kupambana na kundi kubwa la machinga. Tunataka wale maafande waliokuwa wanajiandaa kudhibiti UKUTA ndio wawaondoe machinga. Yaani jiji limekuwa VURUGU TUPU
 
Machinga wa kariakoo halipi ushuru halipi kodi halipii pango..anauza bei rahisi.anapanga biashara mbele ya duka la mtu anayelipia mapato analipa ushuru,pango,mlinzi,stoo,vijana,na EFDS lazima zisome mauzo 5000 kila siku kwa mazingira yale....
 
Yeye ni zaid ya rais aliyesema wakae?.....

Makonda sio credible leader .....

Maagizo yake hayatekelezeki........

Aje na mlejesho ni omba omba wangapi wamerudishwa Dodoma?.....

Bila hivyo bado nitaamini yupo kwenye kundi la watu wanne........
Dodoma ni Mji mkuu so Omba dar ndio panawafaa...
 
Naunga mkono hoja. Kariakoo hakupitiki hata kwa waenda kwa miguu.Machinga wameweka bidhaa njia za waenda kwa miguu..tunapita kwa tabu.
wapelekwe pahala panapostahili kwa biashara.
 
Wamachinga wengi ni vijana wa kiume ambao wengi ni wa kiume ambao hawana 'kazi'...hivi vijana wa kike wasio na kazi huishia wapi????? (NB:...swali langu ni la uchokozi).....
Hili ni swali mujarabu. Pia sio shughuli ya umachinga tu, bali pia udereva na ukonda wa daladala, udereva wa taxi, bajaj, na bodaboda, nk. Ninafikiri kiutamaduni wa kitz, kuna mganyo wa kazi kijinsia za kujitafutia maisha. Mimi nimekuwa nikijiuliza je wasomi wa UDSM hakuna ambaye amelifanyia utafiti hata wa tasnifu ya uzamili au uzamivu na ku-document historia yake, umachinga uliibukaje, ulishamirije, tuko wapi na tunaelekea wapi? Utafiti kama huu unaweza kuwasaidia wanasiasa/watawala wetu kufanya maamuzi ya busara na yenye tija.
 
Na wenye maduka nao,waache kutumia nafasi zilizo mbele ya maduka yao,kupanga bidhaa.Bidhaa zikae ndani ya maduka ili watu waweze kupita kwa urahisi.
 
UKUTA ULIWAFANYA WASEME NDIO HATA ISIPOFAA,saiv wanajiuliza walitoa matamko gani yale tena!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…