Makonda wa Zanzibar kuundiwa tume?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,790
MH.HUSSEIN%20IBRAHIM%20K.%20MAKUNGU.jpg

Hon. Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa)

Mhe.Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa) Mwakilishi na Mbunge amelitaka Baraza la Wawakilishi kuunda Tume ya kumchunguza Mkuu wa Mkoa Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud ambae anajuulikana kama Makonda wa Zanzibar kwa maamuzi yake ya kibabe ikiwemo kuwatia ndani wananchi ovyo kwa utashi wake, kuzivunja nyumba za wananchi kwa sababu za kisiasa.
unnamed%2B%2856%29.jpg

Wwakilishi walisema Mkuu wa Mkoa hana haki wala Mamlaka ya kuwa vunjia wananchi nyumba isipokuwa Mahakama Kuu tu.
 
Naona mheshimiwa Makonda bado kazitawala fikra za watu...

Hata wale wanaojidai eti wana mgomo hata wa kutaja jina lake ndo hao hao kila kukicha hawaeshi kumzungumzia.
hakuna Mheshimiwa anayeitwa Makonda, makonda aliyepo ni mwizi na tapeli wa vyeti na ambaye kwa sasa kwa sababu ya uswahiba tusioujua baina yake na Mkuu wa Serikali ameendelea kubaki madarakani.
 
Mabadiliko ya wakuu wa mikoa yapo mbioni punde na Daud Bashite anapelekwa Kilimanjaro.
 
MBONA MAKONDA NNAYE MJUA HANA TABIA HIZO. NNAYEMJUA NI YULE ALIANZISHA KINONDONI TALENT SEARCH, ALIYE WATAFUTIA WATU AJIRA, KUPITIA JITIHADA ZAKE WATU WENGI WA JIJI HILI WALIPATIWA VIPIMO VYA MAGONJWA MBALIMBALI BURE, ANAHAMASISHA WATU WASIJENGE MABONDENI Etc. huyo wa zanzbar afikii hata sifa hizi
 
Naona mheshimiwa Makonda bado kazitawala fikra za watu...

Hata wale wanaojidai eti wana mgomo hata wa kutaja jina lake ndo hao hao kila kukicha hawaeshi kumzungumzia.

Kumzungumzia sio hoja ila unazungumziwaje ndio shida. Maana hata shetani anazungumzwa sana huko kwenye nyumba za ibada, je naye anasifiwa kwakuwa anazungumzwa?
 
Kumzungumzia sio hoja ila unazungumziwaje ndio shida. Maana hata shetani anazungumzwa sana huko kwenye nyumba za ibada, je naye anasifiwa kwakuwa anazungumzwa?

Mko obsessed na mheshimiwa Makonda nyie...
 
Naona mheshimiwa Makonda bado kazitawala fikra za watu...

Hata wale wanaojidai eti wana mgomo hata wa kutaja jina lake ndo hao hao kila kukicha hawaeshi kumzungumzia.
Ni noma yule dogo hakwepeki hata wasipomtaja kwa vinywa mioyo inamsweat.
 
Back
Top Bottom