Siku za kadhaa kuna habari ambayo Mheshimiwa Makonda kwa kushirikiana na chama wamiliki wa Dalala Dar es Salaam (DARCOBOA) Umoja wa wasafirishaji abiria (UWADAR) na chama cha wafanyakazi madereva (TAWDU) wamekubaliana kuwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke wasafiri bure kwenda na kurudi kazini, hii ni kuanzia saa 11 asubuhi mpaka saa mbili asubuhi na wakati narejea jioni kuanzia saa 9 mpaka saa 11.
Tumezoea kuona haya kwa askari wa majeshi ya ulinzi na usalama, yaani askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Polisi, Magereza na wengine. Pamoja na kuwa kundi hili huwa wako kwenye mavazi maalumu na pia kutokana na unyeti wa kazi Makonda ( makondakta ) wamekuwa wakiwaogopa kidogo, lakini hutoacha kusikia maneno ya kejeli kama tumjaza mawe nk.
Sina uhakika walimu wataepukaje madhira ya kudharirishwa na wahudumu hawa wa daladala ukizingatia wengi wa walimu katika mji mikubwa ni wanawake. Pia sina hakika kama wao wanalifurahia hili,mi nadhani hiyo hela ingelipwa kupitia mishahara yao kwa maana ya transport allowance, au kuwe na mabasi maalumu (staff bus) ikiwa kweli huu mpango endelevu na unalenga kumaliza kero za walimu, lakini pia walimu hawako Dar peke yao na mikoani je itakuwaje? itakuwaje ikiwa mwalimu wa Dar ana high value tofauti na mwalimu wa Pwani?
Tuchukulie mfano, mwalimu atajisikiaje kupanda daladala na mwanafunzi wake, lakini mwanafunzi akilipa nauli na huku akiwa amesimama ili kumpisha mkubwa wake ambaye ni mwalimu?
Katika hili, sitashangaa kusikia zikiibuka kauli za ajabu kutoka kwa makondakta na wengine, hasa wakati watakapokuwa wanakusanya nauli kutoka kwa abiria na kukuta mwalimu akiwa amekaa kwenye kiti, lakini bila kulipa nauli huku mwanafunzi akiwa amelipa na kusimama kwenye daladala.