Makonda umetokea UVCCM, sasa hivi unawatisha watumishi kwa kusema wewe sio mwanasiasa!

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Paul Makonda umetokea UVCCM ghafla sasa hivi unawatisha watu na watumishi wa umma kwa kusema wewe sio Mwanasiasa..

Unawaita watumishi wa umma 'Vichaa' na kuwadhalilisha kwa kauli za kejeli na maamuzi yasiyozingatia utu, haki za binadamu, sheria zilizotungwa na Bunge na katiba ya nchi.

Unafika mahala unataka kuwaaminisha wananchi na watumishi wa umma kuwa uliposimama wewe amesimama Mungu, huko ni kutuingilia vibaya katika imani zetu na kulidhalilisha jina la Mungu ambalo kila alitajae kwa imani yake, analiheshimu.

Unaelekeza maamuzi ambayo sio ya ngazi yako, masuala ya ardhi, elimu, afya, ajira n.k. ni masuala ambayo uwakilishi wake ni ngazi ya Bunge na hoja kuelekezwa serikali kuu na sio TAMISEMI ngazi ya mkoa, masuala ambayo yanaligusa taifa zima ni masuala yanayopatiwa ufumbuzi na mawaziri na sio mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Unafanya maamuzi ya kuwaweka ndani watumishi wa umma na viongozi wa serikali za mitaa kwa amri zako bila kujiridhisha na tuhuma zinazotolewa na wananchi kwa kutumia wataalamu na vyombo vya upelelezi kama Jeshi la polisi, TAKUKURU, n.k.

Unataka kuuaminisha Umma kuwa Tanzania ilipofikia sasa hakuna tena utawala bora unaozingatia sheria za nchi na katiba bali ni utashi wa kiongozi kutumia madaraka yake kumuwajibisha mtendaji aliyekosea kwa kumsweka ndani (rumande) bila mahakama kuthibitisha makosa.

Nilipolizungumza hili siku chache zilizotangulia, wengine waliniambia nimekurupuka kukosoa ziara zako na kwamba hawaniungi mkono.. Sasa nakumbuka usemi wa watu wa kale kuwa 'Mchonga meno, mji umemshinda", ni dhahiri Paul Makonda Dar es Salaam imekushinda na wananchi wanaelekea kukuchoka na kutokukupa ishirikiano.
 
"..., msinijaribu.., Ardhi Kinondoni nitawashughulikia.., hadi mtajuta kuzaliwa..., mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu..., sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama ....kichaa......unanisikia, hauna wa kukutetea.., "
- Paul Makonda (RC), Dar es salaam.
 
Jamani urithi wa majina uendane na sifa za majina hayo.

Paulo na Hapi waliomba ardhi ya Sumaye ifutiwe hati.

Aliyerithiwa jina ye alifanya hivi:

Paulo na Sira waliomba milango ya gereza ikafumguka.
 
"..., msinijaribu.., Ardhi Kinondoni nitawashughulikia.., hadi mtajuta kuzaliwa..., mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu..., sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama ....kichaa......unanisikia, hauna wa kukutetea.., "
- Paul Makonda (RC), Dar es salaam.
... Ametamka haya??
 
Kiburi na majivuno naona yanaongezeka hadi kufikia hatua ya kutaja direct mamlaka iliyojuu ya mamlaka zote!
Maneno aliyoyasema ni makali sana!
 
Jaman ana baraka za mkulu ndomana anatamba na ataendelea kutamba
"..., msinijaribu.., Ardhi Kinondoni nitawashughulikia.., hadi mtajuta kuzaliwa..., mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu..., sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama ....kichaa......unanisikia, hauna wa kukutetea.., "
- Paul Makonda (RC), Dar es salaam.
Huyu mteule sijui alizaliwa kupitia njia ya haja kubwa? Yani anavodhalilisha wazazi wetu ni kama vile yeye kaokotwa choo cha shimo baada ya kuzaliwa na funza badala ya binadamu.
 
Back
Top Bottom