chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Mkuu wa mkoa wa Dar amesema watawarudisha ombaomba wote mikoani kwao na tayari wameshatenga bajeti kwa ajili ya kufanya hivyo na yoyote aliyekwama kurudi muda wowote watamsaidia, na wote watakaoonekana kukaidi watakabiliana na kifungo.
Amesema kwa sasa hivi watakuwa wanawapiga picha na wakimkamata mara ya kwanza na atakapokamatwa mara ya pili watamfunga jela, amesema ombaomba wanapokamatwa wanapigwa faini za 50,000 lakini wanalipa hela hizo bila tabu yoyote jambo linaloonyesha wana hela.
Amewataka kwa wote wanaosema hawana uwezo muda wowote wanaweza kwenda ofisini kwake naatawasiliana mkuu wa mkoa na wilaya wake ili warudi majumbani kwao.