MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ni imani yangu watatii wito huo, wasipofanya hivyo bunge linaweza kuchukulia kama dharau na kulisukuma kumwagiza waziri mkuu kama kiongozi wa shughuli za serikali kuwawajibisha watendaji hao, kwani asipofanya hivyo bunge kwa pamoja linaweza kuazimia kupiga kura ya kutoa na imani nae.
Nina imani wakisimama pamoja basi waziri mkuu anaweza kuondoka kwa sababu akidi haitokua na shaka kutimia na ni kweli ataondolewa.Hapa panaweza kuzua sintofahamu kubwa baina ya mhimili wa dola na bunge, hivyo hili suala linaweza kuonekana dogo lakini ni kubwa.
Serikali pia inaweza kutumia ujanja wa kuzima hili jambo kwa kumuweka Naibu Spika Dr Tulia Ackson ambaye amelalamikiwa sana kufanya kazi kwa maelekezo flani. Naye anaweza kuwafanya wabunge wengi kutoka vyama vyote kumchukia kitu ambacho kinaweza kumfanya akapigiwa kura ya kutokua na imani naye.Achunge sana maana kuna uwezekano mkubwa sana wa yeye kuondoka endapo ataendelea kuzima hoja za wabunge bila sababu.
Ogopa saba bunge likiungana kwa pamoja bila kujali vyama kutetea kitu flani.