Makonda na sakata la madawa ya kulevya

tiku

JF-Expert Member
Oct 31, 2015
441
257
Ndugu wana jf natumaini muwazima , mimi ninapenda kuongelea sakata la madawa ya kulevya .

Mimi naona hakuna binadamu asiyeeleweka kama mtanzania, mwanzo watu walikuwa wanapiga kelele sana kuhusu vijana kuharibika na madawa ya kulevya ambapo hakuna mtu alipenda ile hali nakumbuka wako wati walidai wanaohusika na madawa wakamatwe wanyongwe,

Cha kunishangaza amejitokeza mtu mmoja ameamua kupambana nalo mh Makonda lakini kila mtu anainua mdomo juu kwa kumlaani na kumpinga, hivi kuna mtu gani mwingine hata aliwahi kuthubutu au kujaribu?

jaman huyu jamaa anahitaji kusaidiwa sana mimi naona kwa ushauri ni kipi afanye lakini si kumlaumu hivi hadi kumtukana wakati kizazi chenye nguvu kinaangamia,

Hivi ni nani aliethubutu kujaribu kulifatilia au kulianzisha tangu watu wameangamia na madawa?

Mimi nawashangaa sana watanzania vile hamuelewekagi mnaweza kusema tunapenda ama tunataka hiki mkifanyiwa mnalalamika ,

Kuna mtu anaitwa Mange Kimambi alikuwa mstari wa kwanza kuwalalamikia hawa wauza dawa za kulevya akawa hadi anawataja lakini siku Makonda kaanza hii vita tayari kakurupuka na kumtukana matusi machafu ya nguoni, kweli huyu mwanamke na nyuma yake kuna misukule wengi kweli wanamsaport,

Jaman mimi naomba tumshauri Makonda nini cha kufanya na sio kumvunja moyo vita hii ni ngumu mno maana inahusisha wakubwa wengi sana,

Acha ajirandue tutawapata wahusika tu na watachukuliwa hatua na hilo tatizo litaisha kabisa lakini mkiendeleza midomo midomo wakati mnaona hayupo atayejituma kwa hili hakuna litakalofanyika.
 
Vita gani unataka upigane na migambo tu unakimbia kwenye makomandoo
 
Akiwataja GSM.Ridhiwani na kinje wazawa wa Dar tutamkubali wakuja
Mbona iddi azan zungu kamtaja, angewataja tu sema wa tz bwana wamejaliwa midomoooooo kuvuruga mambo hatawafanyiwe jema aje, hawaridhiki.
 
Wanasema ukitaka kujua tabia au mwenendo wa mtu, angalia mwandiko wake, mavazi yake, mwondoko wake na pengine hata alivyopangilia chumba chake, kitanda chake n.k.

Posting yako inadhihirisha ulivyo na upeo mdogo katika kudadavua yanayojiri katika jamii. Na niseme ni bahati mbaya mno kwamba tuna watu wa namna yako, wasiona kuna kasoro kwa kuwa tu jambo limefanywa na swahiba. Ni bahati mbaya kwa kijana Makonda hata baada ya kuona jamii ilivyoshitukizwa, hajaweza kukaa chini na kutafakari ni nini kimekwenda mrama. Sawa na Siro, afande ambaye alitishwa wakati fulani na Makonda kuhusiana na Shisha, sasa hivi hapendi hata kutafakari hatima ya haya anayosukumiwa. Mwisho wa siku jamii (mimi na wewe) tutalipia yote haya. Wanaotuhumiwa watashitaki na watashinda, kodi zetu ndio zitawalipa. Makonda haoni kwamba ameyumbisha mapambano, anadhani yuko sahihi- katika taaluma ya ufundishaji, tunasema ujuzi sio kukariri na kuonekana kujua kila kitu (kukumbuka!) bali ni kujua chanzo cha taarifa, kuweza kuhoji kwa kutumia vyanzo mbalimbali.

Umenisikitisha tena! Ni kama Makonda alivyonisikitisha - kijana wa leo, anashindwa kuandaa ile orodha fupi tu kwa kuichapisha ili isiwe na ubishi wa kimwandiko- kukaa kitako na kuitaipu (eti anawaambia waandishi wa habari atawapa wao waichape vizuri), lakini orodha isiyo kamili hata chembe, majina ya bandia yasiyo na wenyewe, jina moja moja nk
 
Ridhiwani ni mkazi wa Chalinze-Pwani, Kinje ni mkazi wa Rufiji, Ghalib ni mkazi wa Dubai ndio maana hajawataja
Kama ni hivyo ni ngumu sana kushinda hii vita zaidi zaidi ni kudhalilishana tu, eti kuwakamata watumiaji na wamiliki wa sehemu za starehe !!!!
Binafsi naunga mkono mapambano.
 
ngoja siku moja mtoa mada utajwe kuwa ni muhusika wa madawa ya kulevya utajua watanzania wanalalamikia nini....
 
Ni mpuuzi na mtu asiye na uzalendo pekee atampinga Mkuu wa Mkoa katika vita hii, Ila ni werevu na wenye akili tuu watapinga mbinu/approach iliyotumika, kwani ikiwa tunaamini tutazingatia UTAWALA WA SHERIA, basi ni kuwa vita hii itashia mahakamani na kama itaishia mahakamani Criminal Procedure Act Cap 20 RE 2002, Evidence Act cap 6 Re 2002, Haki za binadamu zilizomo katika katiba na Sheria mpya ya Madawa ya Kulevya No 5 ya mwaka 2015, na Police General Orders zifuatwe ili kusinusuru kesi hizo zikiwa mahakamani, ukiangalia vita hii inavyoendeshwa hauhitaji kusoma sheria kujua kinachofanyika hapa kuwa kimekuwa kikiendeshwa kwa utashi wa kisiasa zaidi kuliko sheria, kuendesha vita hii kisiasa kuliko kisheria zaidi kunadidimisha na kufifisha zaidi vita hii.
 
Ndugu wana jf natumaini muwazima , mimi ninapenda kuongelea sakata la madawa ya kulevya .

Mimi naona hakuna binadamu asiyeeleweka kama mtanzania, mwanzo watu walikuwa wanapiga kelele sana kuhusu vijana kuharibika na madawa ya kulevya ambapo hakuna mtu alipenda ile hali nakumbuka wako wati walidai wanaohusika na madawa wakamatwe wanyongwe,

Cha kunishangaza amejitokeza mtu mmoja ameamua kupambana nalo mh Makonda lakini kila mtu anainua mdomo juu kwa kumlaani na kumpinga, hivi kuna mtu gani mwingine hata aliwahi kuthubutu au kujaribu?

jaman huyu jamaa anahitaji kusaidiwa sana mimi naona kwa ushauri ni kipi afanye lakini si kumlaumu hivi hadi kumtukana wakati kizazi chenye nguvu kinaangamia,

Hivi ni nani aliethubutu kujaribu kulifatilia au kulianzisha tangu watu wameangamia na madawa?

Mimi nawashangaa sana watanzania vile hamuelewekagi mnaweza kusema tunapenda ama tunataka hiki mkifanyiwa mnalalamika ,

Kuna mtu anaitwa Mange Kimambi alikuwa mstari wa kwanza kuwalalamikia hawa wauza dawa za kulevya akawa hadi anawataja lakini siku Makonda kaanza hii vita tayari kakurupuka na kumtukana matusi machafu ya nguoni, kweli huyu mwanamke na nyuma yake kuna misukule wengi kweli wanamsaport,

Jaman mimi naomba tumshauri Makonda nini cha kufanya na sio kumvunja moyo vita hii ni ngumu mno maana inahusisha wakubwa wengi sana,

Acha ajirandue tutawapata wahusika tu na watachukuliwa hatua na hilo tatizo litaisha kabisa lakini mkiendeleza midomo midomo wakati mnaona hayupo atayejituma kwa hili hakuna litakalofanyika.
Mkuu watanzania hatuelewi hata tunataka nini! Tunaongozwa na mahaba ya watu badala ya national interests. Nilitegemea watz tuchimbe mikwara mitandaoni tukionya ole kwa don yeyote atakayethubutu kumgusa Makonda, badala yake tunaongoza kumtishia maisha yake! Makonda amethubutu, no matter amechukua approach ipi, ghafla limeibuka wimbi la ma - experts wa kupambana na madawa ya kulevya wakikosoa kila anachofanya na kuwaunga mkoni washukiwa. Hivi ni nani katuroga? Kabla makonda hajathubutu, hakuna aliyelichukulia serious suala hili, alipoibuka tu, wajuvi wa intelligentsia wakaibuka kumpinga kwa kigezo dhaifu cha "wrong approach."

Mihadarati haina mipaka ya kisiasa wala udini, ina dini yake, serikali yake, mfumo wake nk. Tukikalia kuongozwa kwa itikadi na mahaba niue tutaua kabisa hata hiki kidogo kilichianzishwa.

Kwa miaka 10 kiongozi aliishia kutamka tu kuwa majina ninayo, mwingine ndani ya mwaka amethubutu kuwabainisha washukiwa na kuutikisa mtandao, unadhani ipi ni hatua moja mbele?

Mwacheni RC atekeleze majukumu yake.

Mwenyezi Mungu akulinde katika nia yako njema mheshimiwa RC.

Long live your Excellency Makonda!!
 
Wanasema ukitaka kujua tabia au mwenendo wa mtu, angalia mwandiko wake, mavazi yake, mwondoko wake na pengine hata alivyopangilia chumba chake, kitanda chake n.k.

Posting yako inadhihirisha ulivyo na upeo mdogo katika kudadavua yanayojiri katika jamii. Na niseme ni bahati mbaya mno kwamba tuna watu wa namna yako, wasiona kuna kasoro kwa kuwa tu jambo limefanywa na swahiba. Ni bahati mbaya kwa kijana Makonda hata baada ya kuona jamii ilivyoshitukizwa, hajaweza kukaa chini na kutafakari ni nini kimekwenda mrama. Sawa na Siro, afande ambaye alitishwa wakati fulani na Makonda kuhusiana na Shisha, sasa hivi hapendi hata kutafakari hatima ya haya anayosukumiwa. Mwisho wa siku jamii (mimi na wewe) tutalipia yote haya. Wanaotuhumiwa watashitaki na watashinda, kodi zetu ndio zitawalipa. Makonda haoni kwamba ameyumbisha mapambano, anadhani yuko sahihi- katika taaluma ya ufundishaji, tunasema ujuzi sio kukariri na kuonekana kujua kila kitu (kukumbuka!) bali ni kujua chanzo cha taarifa, kuweza kuhoji kwa kutumia vyanzo mbalimbali.

Umenisikitisha tena! Ni kama Makonda alivyonisikitisha - kijana wa leo, anashindwa kuandaa ile orodha fupi tu kwa kuichapisha ili isiwe na ubishi wa kimwandiko- kukaa kitako na kuitaipu (eti anawaambia waandishi wa habari atawapa wao waichape vizuri), lakini orodha isiyo kamili hata chembe, majina ya bandia yasiyo na wenyewe, jina moja moja nk
Ujuaji mwingi, lakini matendo nil. Long live Makonda
 
Hii vita Makonda tumsupport, naungana naye, nami nishampelekea wauza bangi watano sasa naona vijana wameanza kupona maana unga mitaani haupo kwa sasa.
 
Wanasema ukitaka kujua tabia au mwenendo wa mtu, angalia mwandiko wake, mavazi yake, mwondoko wake na pengine hata alivyopangilia chumba chake, kitanda chake n.k.

Posting yako inadhihirisha ulivyo na upeo mdogo katika kudadavua yanayojiri katika jamii. Na niseme ni bahati mbaya mno kwamba tuna watu wa namna yako, wasiona kuna kasoro kwa kuwa tu jambo limefanywa na swahiba. Ni bahati mbaya kwa kijana Makonda hata baada ya kuona jamii ilivyoshitukizwa, hajaweza kukaa chini na kutafakari ni nini kimekwenda mrama. Sawa na Siro, afande ambaye alitishwa wakati fulani na Makonda kuhusiana na Shisha, sasa hivi hapendi hata kutafakari hatima ya haya anayosukumiwa. Mwisho wa siku jamii (mimi na wewe) tutalipia yote haya. Wanaotuhumiwa watashitaki na watashinda, kodi zetu ndio zitawalipa. Makonda haoni kwamba ameyumbisha mapambano, anadhani yuko sahihi- katika taaluma ya ufundishaji, tunasema ujuzi sio kukariri na kuonekana kujua kila kitu (kukumbuka!) bali ni kujua chanzo cha taarifa, kuweza kuhoji kwa kutumia vyanzo mbalimbali.

Umenisikitisha tena! Ni kama Makonda alivyonisikitisha - kijana wa leo, anashindwa kuandaa ile orodha fupi tu kwa kuichapisha ili isiwe na ubishi wa kimwandiko- kukaa kitako na kuitaipu (eti anawaambia waandishi wa habari atawapa wao waichape vizuri), lakini orodha isiyo kamili hata chembe, majina ya bandia yasiyo na wenyewe, jina moja moja nk
Wewebnjilembera ni mmojawapo wa wahusika wanaoharibu kizazi hiki na madaw ya kulevya yaani wewe ni punda mbeba unga kwasababu huwezi kujifanya mstaarabu ktk hili nakuona nimekosea bwege mkubwa nakwambia misho wenu umefika, ungekuwa muungwana ungeshauri nini chakumshauri makonda afanye ili kubotesha vita hii sio kuropoka tu nakujifanya ujuaji, na uitaka kujua wewe hamnazo unaanza kuangalia uandishi wangu, mfyuu nasikitika watanzania amba akili zao zipo miguuni
 
Usitishwe na uandishi wangu sijazoea kutumia smart phone nineanza kutumia juzijuzi tu so kukosea speling sio shida.
 
Kaka kuna harufu ya madon Wauza unga wanaotaharibia watoto zetu kuwanunua waheshimiwa pale Mjengoni...
 
Mkulu wa kaya kesha tatua swala la Mhs Makonda baada ya kumuweka Comissioner tume na wasaidizi wake!!
Hivyo sasa taratibu zitafuatwa ktk utekelezaji wa opps hizi!!
Makonda tunampongeza kwa uthubutu wake! Info zote juu ya kadhia hii amshirikishe mkuu wa kitengo na team yake!!
 
mimi nilishawai andika uzi kama huu wako mzee,hakuan mtubwa ajabu huku duniani kama Mtanzania maana huwe elewa anataka nn na wakati gani,na wanachopigia kelele ni mwenyekiti wao chadema kutajwa na si kingine
 
Back
Top Bottom