Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Mh. Paul Makonda,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,nakusalimu. Ndugu Makonda,umesikika ukisema kuwa umewaajiri wanasheria saba kwa kuwasaidia wananchi kwenye kuingia mikataba au kufungua kesi kwenye mahakama. Ingawa wazo na nia yako ni njema,umedhalilisha tasnia ya sheria.
Umesema kuwa unawalipa wanasheria hao asilimia sabini na tano ya mshahara wako kwa mwezi. Pamoja na kutojua mshahara wako kwa mwezi,nina hakika asilimia hiyo haiwezi kuwalipa wanasheria saba. Tasnia ya sheria ni moja ya tasnia kongwe,adhimu na ghali hapa duniani. Madai yako yanaidhalilisha tasnia hii ya sheria. Wanasheria saba walipwe asilimia 75 ya mshahara wako!? Hakika hiyo ni dharau.
Ndugu Makonda,najua wewe ni mwanasiasa na kiongozi wa kiserikali. Kauli zako zinapaswa kuchujwa vyema kabla ya kutolewa. Kwa taarifa yako,hakuna wanasheria saba wanaoweza kuajiriwa kwa mshahara wa kiudhalilishaji kama huo. Hata wanafunzi wa sheria huwezi kuwapata,seuse wanasheria.
Natoa rai kwako Ndugu Paul Makonda kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi wanasheria wa nchi hii kwa kauli yako ya kushusha thamani yao. Nikiwa mwanasheria,nimeshtushwa na kusikitishwa na kauli yako.