Makonda awatetea wanaume wa Dar

Makonda awatetea wanaume wa Dar

Nyie watu mnanikera kweli kweli. Mbona mnajikombakomba?

Sisi WANAUME WA DAR, tulizaliwa OCEAN ROAD na MUHIMBILI na sio Bugando na mapori mengine ya akiba au sijui Same au Mwanga huko Store Mombasa au Kiruru Ibweijeiwa kwa kina
Mshana Jr

Kama Dar ulikuja wewe ni WAKUJA. Na kwa taarifa yenu, tumezaliwa chips tukiziona na hatuna ajabu nazo, SISI NDIO TUMEZIUMBA.

Nyinyi WAKUJA, mkifurumuka kutoka kwenye mapori ya akiba huko mkafika Dar kuja kuosha macho, hamtaki kurudi kwenu. Mkifika hapa mnafakamia chips mayai kwa pupa na kujisahau. Mnavaa nguo spesho kama waimba kwaya na wengine mnachangammmmmka kuliko sisi wenyeji wenu. Saa zote mna earphones masikioni hata tukiwapigia honi mtupishe hamsikii. Kitu mnachosikia haraka ni kengele za baiskweli.

Mwanaume wa Dar ni yule mzaliwa waDar na sio nyinyi mnaotujazia jiji kwa kuwa tu mtandao wa barabara za lami umeimarika.

Huko mlikotoka saa zote mkiwa mashambani na kwenye mapori yenu ya akiba mnashinda mkitafuna mzizi huu mara huu. Lkn mkija hapa mnatusingizia eti hatuamshi dude hadi kwa mizizi...hebu acheni urongo, hii mizizi inayoletwa huku na wamasai ni kwa ajili yenu. Mlikuwa mkiila mkiwa huko na sasa mmehamia mjini wenzenu wanawaletea muendelee kupona, lkn kwa kuwa mkija huku mnajibrand eti na nyie ni Walume wa Dar, basi mnatuchafua.

😂😂😂😂😂eti mapori ya akiba..nimecjheka jaman
 
Niambie chaurongo...msomi wa kadi la kliniki. Mbwembwe nyiiiiingi kumbe ulizaliwa pori la akiba! Sasa unaona shida ya urongo? Huko ulikozaliwa mkunga wa kienyeji alitoa wapi kadi?
Mkuu nimezaliwa mjini nimekulia mtaani nazeekea porini SIO WOTE TUMEZALIWA MAPORI YA AKIBA! usikariri basi!
 
Ulitakiwa ata iyo avatar uibadilishe ujiite mwana mtoka pazuri tu. Hakuna mwanaume wa dar ambaye ni bad boy mtoka pabaya. Watoto wazuri tu nyieeee
Hata avatar yako inasadifu wajihi wako. Umetoka pori la akiba la Mkoreha hukooo Tandahimba, umefika Dar unajiita Tupac...tunasingiziwa sisi.

Television zilianzia hapa mjini, hatuna jipya nazo. Kazi ipo kwa WAKUJA...mnavaa majaketi Dar na joto hili, bonge la kiatu na jeans nzito. Mnatutia aibu
 
Ulitakiwa ata iyo avatar uibadilishe ujiite mwana mtoka pazuri tu. Hakuna mwanaume wa dar ambaye ni bad boy mtoka pabaya. Watoto wazuri tu nyieeee
Tozi tu wewe, mvaa nguo za dukani. Mkija town mnakurupuuuuuka na hereni, earphones na maviatu makubwaa huku mnanuka miguu. Wenyeji tunawaangalia tu.

Ndio maana mkiingia tu kitaa tunawasachi kuwatoa ujinga. Ukija mjini njoo ufikie kwangu nikupe madarasa sharo, sawa?
 
Hata avatar yako inasadifu wajihi wako. Umetoka pori la akiba la Mkoreha hukooo Tandahimba, umefika Dar unajiita Tupac...tunasingiziwa sisi.

Television zilianzia hapa mjini, hatuna jipya nazo. Kazi ipo kwa WAKUJA...mnavaa majaketi Dar na joto hili, bonge la kiatu na jeans nzito. Mnatutia aibu
Mkuu hapo kwny avatar umenigusa kidogo. Hanna MTU aliyezaliwa Dar akajiita tupac, Nelly. Ebu cheki avatar yako Mwana mtoka pabaya. Cheki na yangu Simba Songea..haya majina ya kizungu kwa wanaume wa Dar ni expired
 
1543837444630.png

Mkee na wewe ni wa dar?
 
Mkumbusheni kwamba hakuna hajja ya kuoa pia Maaana akienda Kimboka huduma inapatikana hata kwa elfu 2
 
Back
Top Bottom