Makonda Angalia jinsi Marais Duniani wanavyotaniwa

Carica_papaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
758
1,232
images (3).jpeg
 
Hiyo ni marekani,kuna hadi porn mtu kavaa sura ya obama, usilinganishe sana huko na huku
Anyway kuhusu makonda kuwa sahihi sijui
 
Uhuru wa kutoa maoni bado sana bongo.
Kitu ambacho watawala wetu hawajui ni kwamba, ukiwapa watu uhuru wa kutoa maoni, unawafaidisha wao wananchi, na wewe mtawala unafaidi.

1. Unawafaidisha wananchi kwa kuwapa uhuru wao wa kikatiba.

2. Kisaikolojia, mtu anayeonewa lakini akaachiwa uhuru wa kusema kaonewa ana uwezo mkubwa wa kusamehe ma kuendelea na maisha kuliko mtu ambaye kaonewa, halafu kanyimwa uhuru wa kujieleza. Unaweza kuzuia mapinduzi ya kijeshi kwa kuwapa watu uhuru wa kujieleza.

3. Kiintelijensia, ni rahisi kuwafuatilia na kuwadhibiti watu waliopewa uhuru wa kujieleza kuliko waliobanwa. Watawala kubana uhuru wa kujieleza wanajibania wenyewe nafasi za kupata taarifa.

4. Kiutendaji, kunyima watu uhuru wa kujieleza ni kuminya njia za kupata feedback kutoka kwa wananchi. Uongozi utashindwa kujitathimini kutokana na maoni ya moja kwa moja na ya kweli ya watu. Hii ni moja ya sababu Soviet Union ilianguka. Viongizi walikuwa wanaandikiwa ripoti za maendeleo za uongo tu. Mpaka Gorbachev akasema huu ujinga, hatuwezi kuendelea hivi.

5.Kuminya uhuru wa maoni kunaikosesha serikali nafasi ya kujibu hoja za wanaoisema vibaya. Nchi yenye uhuru wa kutia maoni, serikali ikishambuliwa kwa uongo, watu wanasema wazi, serikali inaoata nafasi ya kujibu tuhuma. Inajibu. Kama hakuna uhuru wa kutoa maoni, serikali inasemwa vibaya chinichini, hata kwa uongo, na uongo unaaminika kuwa ukweli. Kwa sababu serikali haipati nafasi kukanusha. Kwa sababu nchi imekosa uwazi watu wanasema chinichini.
 
Back
Top Bottom