Makonda Angalia jinsi Marais Duniani wanavyotaniwa

IMG_20191101_180007.jpg


Angalia hiyo
 

Usinakili kila kitu eti kwasababu wengine wanafanya, nchi hii ina mila, desturi na miiko yake mambo ya kipuuzi puuzi msilete kusema eti ndo uhuru, tafadhali tuwe makini katika matendo yetu tusijekugharamika, uhuru tulionao tusiutumie vibaya, unajua heshima ya kiti cha Mh Rais?, ile alama iliyopo pale kwenye kiti sio pambo au ua lingine lakawaida, pale ndipo panapotoka mawazo ya hekima na busara ya kuongoza nchi. uhuru upo ila USIVUKE MIPAKA
 
............mzaha mzahaaaa HUTUMBUA USAHaaaa..... 🙌 🙌
 
Mkuu ,sijui kwanini umeniuliza hilo swali,anyway labda hukuelewa nilichoandika
Kuhusu hiyo picha uliyoweka,kwani unamjua aliyeitengeneza ? Na ina miaka mingi zaidi ya tisa wakati ule hatukua na hiyo sheria
Nakuuliza tena
Hivi unajua Tanzania kwa sasa ina zaidi ya watu 50M??
Kabla ya kutetea unachokitetea hivi umeshawahi kusoma hivi vitabu??
images (9).jpeg

images (7).jpeg

images (8).jpeg

images (10).jpeg
 
Kitu ambacho watawala wetu hawajui ni kwamba, ukiwapa watu uhuru wa kutia maoni, unawafaidisha wao wananchi, na wewe mtawala unafaidi.

1. Unawafaidisha wananchi kwa kuwapa uhuru wao wa kikatiba.

2. Kisaikolojia, mtu anayeonewa lakini akaachiwa uhuru wa kusema kaonewa ana uwezo mkubwa wa kusamehe ma kuendelea na maisha kuliko mtu ambaye kaonewa, halafu kanyimwa uhuru wa kujieleza. Unaweza kuzuia mapinduzi ya kijeshi kwa kuwapa watu uhuru wa kujieleza.

3. Kiintelijensia, ni rahisi kuwafuatilia na kuwadhibiti watu waliopewa uhuru wa kujieleza kuliko waliobanwa. Watawala kubana uhuru wa kujieleza wanajibania wenyewe nafasi za kupata taarifa.

4. Kiutendaji, kunyima watu uhuru wa kujieleza ni kuminya njia za kupata feedback kutoka kwa wananchi. Uongozi utashindwa kujitathimini kutokana na maoni ya moja kwa moja na ya kweli ya watu. Hii ni moja ya sababu Soviet Union ilianguka. Viongizi walikuwa wanaandikiwa ripoti za maendeleo za uongo tu. Mpaka Gorbachev akasema huu ujinga, hatuwezi kuendelea hivi.

5.Kuminya uhuru wa maoni kunaikosesha serikali nafasi ya kujibu hoja za wanaoisema vibaya. Nchi yenye uhuru wa kutia maoni, serikali ikishambuliwa kwa uongo, watu wanasema wazi, serikali inaoata nafasi ya kujibu tuhuma. Inajibu. Kama hakuna uhuru wa kutoa maoni, serikali inasemwa vibaya chinichini, hata kwa uongo, na uongo unaaminika kuwa ukweli. Kwa sababu serikali haipati nafasi kukanusha. Kwa sababu nchi imekosa uwazi watu wanasema chinichini.
MKUU HII HAIPASWI KUWA COMMENT BALI THREAD UMETEMA LECTURE YA MAANA ,BIG UP
 
Back
Top Bottom