Makonda anatafsiri Biblia vibaya ndio maana anakosea

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Ndugu zangu huu ni ushauri wa bure ambao unaweza kumsaidia kijana mwenzetu kuendelea kuwatumikia wanchi vizuri bila kuwa na misuguano isiyo na lazima.

Nimesikiliza kwa makini clip ya ndugu yangu alipokuwa kanisani na kunukuu kifungu cha Biblia katika KUTOKA 14:13-16"Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakao wafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya. BWANA akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israel waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyooshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israel watapita kati ya bahari katika nchi kavu

Kama utasikiliza kwa makini anachongea kijana wetu ni tofauti na kilichoandikwa kwenye Biblia. anasema kuwa Mungu alimwambia Musa apige bahari kwa fimbo yake siyo kweli Mungu alimwambia Musa anyooshe fimbo yake kuigawa bahari. Kwa mtazamo huo kijana wetu anapiga mahali ambapo anatakiwa kunyoosha tu, hivyo ndivyo alivyofanya Musa kinyume na maelekezo ya Mungu na adhabu yake alikataliwa kuingia Kanani. Mungu alimwambia Musa auambie Mwamba utoe maji yeye akaupiga mara mbili kwa fimbo Mungu akamwambia hataingia kwenye nchi ya ahadi, ingawaje maji yalitoka.

Jambo la pili Mungu ambaye ni Yehova wanayemwabudu Wakristo ni tofauti na Mungu Allah wanayemwabudu Waislamu. Wakristo wanaamini Mungu wa kwali lazima aabudiwe kupitia Yesu Kristo kama ilivyoandikwa katika

Matendo 4:12,wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote,kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwao.matendo 2:21,na itakua kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.Yohana 14:6,Yesu akawaambia,Mimi ndimi njia,na kweli na uzima;mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya Mimi. Kwahiyo kutokana na maandiko haya Wakristo wanaamini hakuna nabii au mtume mwingine anayeweza kumsaidia mwanadamu kumuona Mungu Yehova kinyume na hapo ni miungu kama ya Baali

Waislam wanaamini kuwa Mtume Muhamad ndiye mtu wa mwisho aliyekuja kuwakomboa wanadamu na kuwaandalia njia ya kumuona Allah, sasa kijana mwenzetu anajaribu kushikilia kote kote jambo ambalo Biblia imekataza lazima afanye uamuzi wa kuchagua ni yupi anayemwamini kumsaidia la sivyo anaipinga

Biblia 1Wafalme 18:21 Kisha, Elia akawakaribia watu hao, akawaambia, “Mtasitasita na kuyumbayumba mioyoni mpaka lini? Ikiwa Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu mfuateni; lakini ikiwa Baali ni Mungu, basi, mfuateni yeye.” Lakini watu hawakumjibu neno lolote.

Usinukuu Biblia vibaya kuhalalisha matakwa yako utaingia kwenye mgogoro na Mungu.
 
- Kumbe hapa Bongo tuna Miungu anayejua nani anatafsiri Biblia sawa sawa na nani anakosea? Duh JF bwana siku hizi inao mpaka Miungu U know hahahahahahaha

le Mutuz
 
Mwambie Boss wako aonyeshe vyeti banaaaa. Hilo ndio la msingi kwa sasa. Mambo ya biblia tuwaachie walioitunga!
 
- Kumbe hapa Bongo tuna Miungu anayejua nani anatafsiri Biblia sawa sawa na nani anakosea? Duh JF bwana siku hizi inao mpaka Miungu U know hahahahahahaha

le Mutuz

upload_2017-3-6_15-4-36.jpeg
 
- Amuonyeshe nani vyeti? hahahahahahahahha

le Mutuz
Sisi wananchi tunataka tuone. Maana sasa tunamchukulia kibashite bashite mpk watoto mtaani wanamkebehi. Mwambie arudishe heshima yake irudi. Mimi naamini vyeti vyake havina tatizo lolote..basi atuthibitishie baaas..tuendeleze vita ya madawa maana sasa imedorora!
 
- Wewe na nani hasa kwa mfano? hahahahahahahha

le Mutuz
 
Back
Top Bottom