Makonda ana kosa la kujibu

Makonda ana kosa la kujibu

Dindira

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Posts
2,912
Reaction score
3,469
Kwanza alidanganya kwamba aliingiza mzigo wenye vifaa vya shule kumbe ndani kuna matrekta na mashine za kunyunyizia dawa shambani. Hivi sio vifaa vya walimu wa Dar es Salaam.
Pili.. Yeye kama mtumishi wa umma hapashwi kupokea zawadi binafsi. Hiyo itakua ni rushwa haina jina jingine. Ukipewa zawadi inayoingia kwenye kontena 20. Hao waliokupa utawalipa nini ?
 
Anatumbuliwa jumatatu tar 3 mwezi wa 8 saa 4:43 asubuhi tena akiwa anaendelea na shughuli fulani...so sad.
 

Nasikia Kitwanga alitumbuliwa kwa kujibu swali akiwa amelewa.​
 
Picha imekaribia kuishaaaaa(in Soudybrown's voice)
 
Kwanza alidanganya kwamba aliingiza mzigo wenye vifaa vya shule kumbe ndani kuna matrekta na mashine za kunyunyizia dawa shambani. Hivi sio vifaa vya walimu wa Dar es Salaam.
Pili.. Yeye kama mtumishi wa umma hapashwi kupokea zawadi binafsi. Hiyo itakua ni rushwa haina jina jingine. Ukipewa zawadi inayoingia kwenye kontena 20. Hao waliokupa utawalipa nini ?
Hivi kuna mpaka Matrekta ndani.
Siamini kama kuna kiongozi angeweza anaweza kufanya uhuni huo awamu hii bila kushughulikiwa. Huonda ni ishu inayojulikana au kuna wapambe nyuma yake .
Lakini pia kama ni kweli kuwa kuna Matrekta basi ni vizuri Bunge lijalo likaunda Tume ya kulichunguza suala hili kwa undani.
Kuna jambo kubwa limefichika nyuma yake.

Hua ni kawaida kwenye manunuzi makubwa kama ambayo yamefanyika kwa kipindi hiki ,makampuni yanayoingia mikataba wanatoa kamisheni Fulani kama shukrani ya kuwaunganishia biashara zao.
Sasa huenda Kamisheni hizo imekua vigumu kuziingiza kama fedha Taslim kutokana na awamu hii kujipambanua kuwa inapambana na ufisadi badala yake wajanja wakaangalia namna ya kuziingiza kidogo kidogo huku wakijifanya kuwa wanasaidia kununua makochi ya walimu kukalia darasani.

Hii misaada inayeoingia kupitia watu binafsi inabidi serikali iwe macho sana.

Kuna ishu nyingine ya Ujenzi wa Chuo cha VETA kupitia Musiba kwa kauli zake za kuunga mkono serikali.
Eti watanzania waishio Marekani wanataka kujenga Chuo Kikubwa cha VETA kuliko vyote kusini mwa jangwa la sahara.

Chuo kikubwa kama Cha Chang'ombe kinahitaji mabilioni mengi sana ya fedha. Ukubwa wa chuo ni miundo mbinu. Miundo mbinu ya vyuo vya ufundi ni gharama kubwa sana. Je ,kuna watanzania waishio Marekani wameona biashara kubwa ya VETA wakaamua kuwekeza au ni wajanja wachache wanakuja na mbinu zao za kutakatisha Fedha hasa baada ya kuona awamu hii imejitahidi kubana uingizwaji wa fedha haramu zinazotokana na takrima kwa baadhi ya watendaji kupewa asante.

Kwa sababu tujiulize tu Mawaziri hawajatoka toka huko nje hasa Marekani na pia Rais wetu hajawahi kusafiri kwenda nje ya bara la Afrika sasa hayo mazawadi nani anapewa na anapewa kwa makubaliano gani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutaongea mpaka povu lituishe sijaona wa kutumbuliwa. Kumbukeni waliotumbuliwa wote ilikuwa ni kwa staili ileile moja ya hapo kwa hapo.
Lakini hii ngoma imelala na hivyo imeshadunda. Mtahesabu siku mpaka mtasahau wenyewe
 
soon anaenda kubadilishiwa majukumu ila sio kutumbuliwa
 
Kwanza alidanganya kwamba aliingiza mzigo wenye vifaa vya shule kumbe ndani kuna matrekta na mashine za kunyunyizia dawa shambani. Hivi sio vifaa vya walimu wa Dar es Salaam.
Pili.. Yeye kama mtumishi wa umma hapashwi kupokea zawadi binafsi. Hiyo itakua ni rushwa haina jina jingine. Ukipewa zawadi inayoingia kwenye kontena 20. Hao waliokupa utawalipa nini ?
Matrekta ni kwa ajili ya mashamba ya shule za dar... Kumbuka dhana ya kilimo kwanza
Mashine ni kwa ajili ya kufanyia fumigation mashuleni.. Kumbuka vita dhidi ya malaria.....
Sema tu MASOFA (makochi laini) hayakuonekana! Je hili lilikuwa kachumbari kwenye roast?

Jr[emoji769]
 
Acha kupotosha umma, sisi tulikuwepo. Yale matrecta siyo ya makonda ni Mali za watu wengine walioshindwa kulipia ushuru pale bandarini. Ukome kueneza Habari usioijua. Wewe ni mpuuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuu[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji144] [emoji144]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom