Makonda alipanga kuvuruga shughuli ya Joketi

Makonda alipanga kuvuruga shughuli ya Joketi

Katika adhara Kama ile iliyowaleta Watanzania kwa pamoja na Makonda akiwa mwalikwa tu sikutegemea kuona kwamba wapo walioalikwa kwa umuhimu kuliko wengine.

Kauli ya Makonda dhidi ya waalikwa wenzake inaweza isieleweke ila ina tafsiri kwamba wapo wanaostahili kuingia kwenye karama na ambao hawastahili kuwepo kwenye karama Kama ile.

Inatufundishwa kwamba lipo gape kubwa la wanalionacho na wasionacho,masikini na matajiri na Hawa watu hawapaswi kuwa pamoja.

Naamini watoto wa kike wanaotafutiwa elimu Bora huko kisarawe ni watoto wa walevi, watoto wa watu wa ovyo kama tafsi ya Makonda ilivyo nk
Kama tunalenga kuwasaidia, je ni sahihi hao watoto wakawaona baba zao kuwa ni watu wa ovyo? Ni sahihi kutumia michango yetu kuwadhalilisha watoto wa kike wanaotokana na familia za ovyo Kama anavyowaita Mkuu wa Mkoa.

Ni kauli nyepesi kwa wasiofikiri kuhusu utu lakini ni kauli ya ubaguzi kwa wanaotambua thamani ya utu na ubinadamu.....Taifa letu linatuhitaji wote kwa wakati mmoja, si Taifa la matajiri na wenye madaraka bali ni taifa la Watanzania.

Leo Piere angechukua microphone akasema mkuu wa mkoa ni mtu wa ovyo mngemwacha? Kwanini mkuu wa mkoa amtukane mtu Tena mbele ya vyombo vya habari na tukae kimya? Yeye ni Nani kwenye nchi yetu Hadi aweze kujua nani wa ovyo na asiye wa ovyo? Anajua wanagapi wanapata riziki kwa anachofanya Piere?

Jana Pieere katoa laki moja, je wangapi wenye nazo na wamesikia uhamasishaji na wengine anaowaona wa muhimu kwake lakini hawakutoa hata shilingi moja wala kuhudhuria?

Nadhani Joketi amevunjwa moyo na aliyemtegemea, hiyo afla angeandaa Makonda na kumwalika konki angeweza kumtukana?

Joketi alimwona wa maana akamwalika wewe unayemwona wa ovyo uhitaji kumwalika kwenye Mambo yako...

Inaumiza Sana kuwaona binadamu wenzako Kama vinyago flani

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna ukweli
 
Kwa uelewa wangu mimi mtu wa ovyo ni binadamu yoyote anaefanya matendo yasioyokubalika kwenye jamii husika.Mfano wasaniii wote wanaoimba nyimbo za matusi ni watu wa ovyo,wasanii wote wanaoweka picha za utupu kwenye mitandao ni watu wa ovyo,wasanii wote wanaonengua kwa kushika maeneo yao nyeti ni watu wa ovyo.
je,mwigizaji nae aneigiza ulevi ni mtu wa hovyo?je wanaotoa kauli za kijinga pia si wa hovyo???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kiukweli DC nae anamwalikaje mtu mwenye zero kwenye taluma yake aende kwenye tamasha la tokomeza zero?

Makonda jipime na ujipime haswa kuna dalili ukapata pigo kutoka kwa Mungu mwenyewe maana mteule wako yupo kimya kwa sifa za kijinga ulizonazo.

Mda sio rafiki ila ni kipimo sahihi pale mda utakapo ongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu mimi mtu wa ovyo ni binadamu yoyote anaefanya matendo yasioyokubalika kwenye jamii husika.Mfano wasaniii wote wanaoimba nyimbo za matusi ni watu wa ovyo,wasanii wote wanaoweka picha za utupu kwenye mitandao ni watu wa ovyo,wasanii wote wanaonengua kwa kushika maeneo yao nyeti ni watu wa ovyo.
Hata wanaofoji vyeti wakati walipata division zero ni watu wa hovyo, kinachotushangaza sisi ni kwanini uangalie kibanzi kwenye jicho la mwenzako wakati wewe una mboriti ???
 
Tatizo la kuteua mkuu wa mkoa ambaye hafai hata kuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi.
 
Mimi ni shabiki wa Makonda sana ila kina baadhi ya mambo kumtetra inakuwa ngumu sana. Si vibaya akaomba radhi kweli amekosa hata kama ni kweli Makonda ajue kuwa Yesu alikuja kwa wenye dhambi kuwaokoa si watakatifu au yeye anasoma Bible ipi? Kwa hili MZEE baba Mimi shabiki ako umechemka Sana japo wewe huwa mgumu kuomba msamaha hapa omba ndo uungwana. Acha kushikilia misimamo isiyo na tija.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom