Makinda: Wabunge EALA ruksa CHADEMA style | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda: Wabunge EALA ruksa CHADEMA style

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 27, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amewataka wabunge wa Tanzania wanaowakilisha katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kususia vikao na kutoka nje pindi wanapoona sheria zinazopitishwa na Bunge hilo, zinaweza kuhatarisha taifa. Spika Makinda alisema hayo juzi usiku wakati wa kufunga semina elekezi kwa wabunge hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kanuni ya kutoka nje kwa wabunge hao lazima izingatiwe pale wanapoona kushindwa kutetea jambo lenye masIlahi kwa nchi.


  Spika Makinda, alisema kanuni ya kutoka nje lazima waitumie hasa pale wanapoona hoja walizotoa zimeshindikana kwa kuwa wasipofanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuuza nchi. “Nyinyi mpo tofauti na wabunge wa hapa nchini kwa kuwa mnawakilisha zaidi ya Watanzania milioni 50 katika Jumuiya hiyo, hivyo suala la kutoka nje lazima mlitumie pale mnapoona inafaa, maana wale wenzenu wana umoja sana,” alisisitiza.


  Spika Makinda alitoa msisitizo huo baada ya mratibu wa Bunge la EALA kwa Tanzania, Justina Shauri, alipowasilisha mada akiwataka wabunge hao kutumia staili ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutoka nje pindi wanapoona hawatoshi katika kura zao. Aliwataka wabunge hao kujitambua na kuwa wavumilivu katika kila jambo kwa kuwa wakiharibu wanakuwa wameivuruga nchi. Alisema kutokana na uvumilivu na kutokuwa mjuaji ndiyo maana ameweza kudumu katika ubunge na mwaka 2015 anatimiza miaka 40 ya ubunge wake.


  Spika Makinda alisema kuwa kwa kawaida wabunge wapya wanakosa uvumilivu, huku akitolea mfano bungeni Dodoma ambapo kuna wabunge wengi vijana na wapya, ambapo tangu siku ya kwanza wanajua, wakati kiongozi si kila mara unatakiwa kusema. Alisema kutokana na kukosa kuzijua kanuni mara nyingi hujisikia vibaya pale anapomwambia mbunge akae chini wakati wananchi wake wanamtazama kupitia televisheni.“Nilipoingia bungeni nilikuwa mdogo sana lakini kwa miezi sita sikuzungumza lolote...ili uweze kuzungumza ni muhimu kuzijua kanuni, kwa kuwa Bunge linaongozwa kwa kanuni,” alisema.


  Hata hivyo akichangia katika hoja ya kutoka nje, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukhindo (CCM), alipingana na kauli hiyo na kuwataka wabunge hao kuwa waangalifu na kuacha kususia kila kitu, kwani wakifanya hivyo wenzao kwa umoja wao wataendelea kutekeleza majukumu yao. Naye, mbunge mteule, Makongoro Nyerere, alipinga staili hiyo ya CHADEMA na kusema kuwa kama kuna hoja basi wabunge hao hawatapaswa kutoka nje. “Leo umepigania nafasi na kupata, sasa kama una hoja kwa nini utoke nje? Tumia nafasi hiyo kusema, maana ukitoka nje utakwenda kusemea kijiwenim, hivyo kususia hatuombei, tupo pale kujenga hoja na tutaweza...Mungu tusaidie,” alisema.


  Kwa upande wake mbunge wa EALA anayemaliza muda wake, Kate Kamba, alisema kuwa kutoka nje kunaruhusiwa kikatiba kwa ibara ya 13, hasa kwa suala lenye masilahi ya nchi. Hata hivyo Spika Makinda amekuwa akipingana na tabia hiyo inayotumiwa na wabunge wa CHADEMA ambao wamekuwa wakitoka nje ya vikao pamoja na kususia mijadala mbalimbali bungeni mjini Dodoma.   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Speaker Makinda amekuwa akipinga vikali mtindo wa wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge pindi taratibu zinapopindishwa au kutokukubaliana na hoja fulani, au kushinikizwa na wabunge wengi wa CCM. Iweje leo aridhie Chadema Stile kuwashinikiza wabunge East Afrika wanaotoka Tanzania kupinga au kutokukubaliana kwa mtindo huo? Hii ni dalili tosha huhu mama anaendesha bunge kisanii badala ya kufuata taratibu na sheria.
   
 3. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Awataka wabunge wa EAC upande wa Tz kutumia staili ya chadema kutoka nje ya bunge (kususia) pale wanapoona dalili za kuburuzwa na wenzao kutokana na idadi yao, amesahau kashfa zake kwa makamanda?

  Au alikuwa anafagilia kimyakimya?
   
 4. U

  UmtwaAlumbwagwe Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyasema lini tena hayo? Nijuze tafadhali
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  She admires CHADEMA!
  Wanamkosesha usingizi!
   
 6. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hiyo mbinu inaruhusiwa mahali popote pengine siyo kwenye magamba
   
 7. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Kitu nilichojifunza leo ni kwamba kumbe CDM walikuwa sahihi walipokuwa wanatoka nje ya ukumbi wa bunge pale wanapogundua kuna mswada magumashi. Hii ni kutokana na kauli ya Anna Makinda akiwaambia wabunge wa Afrika mashariki kwamba ni rukhusa kugoma endapo watagundua majadiliano hayana maslahi kwa jamii. Kilichonishangaza ni kwamba wakati CDM wanagoma alikuwa akiwatolea lugha ya kejeli wakati CDM ilikuwa ni msimamo wao.
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kumbe mother alikuwa anadesa?
  nimeamini hakuna aliyekamilika kila siku tunajifunza.
   
 9. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kweli ukiwa mtumwa sana unasahau hata watu unaoongea nao..... Hivi huyu mama yeye alikuwa anadesa tu bungeni miaka yote na anataka pia wabunge wa EALA wakatulie tuli na huko.........

  kweli aibu hii sijui itaisha lini........
   
 10. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,763
  Likes Received: 8,036
  Trophy Points: 280
  Kumbe anajua MALE ACTS
   
 11. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Katika mfululizo wa kuwafunda Wabunge wa EALA(Bunge la Afrika Mashariki) jana ilikuwa zamu ya Madam Makinda baada ya Samwel Sitta! Makinda aliwakumbusha wabunge hao umuhimu wao ktk bunge hilo,akawakumbusha kuwa wanawajibika ktk bunge la Tanzania,wawe wazalendo,watetee maslai ya nchi na watanzania kwa ujumla wake...Katika kutia msisitizo Spika Makinda akasisitiza Bungeni si mahali pa watu wahuni,wenye kuleta picha mbaya kwa jamii,akaendelea kusema ni aibu kwa Mbunge kuandikwa ktk media yupo club za usiku,au anatuhumiwa kwa ufuska na tabia zinazoendana na hayo..ktk kujazia nyama Makinda akamtaja Shy-Rose Bhanji,akamsihi abadilike..tena akahoji..iweje Bhanji ajipeleke ktk ubalozi wa Kenya wakati bado hajaapishwa kama Mbunge wa EALA?Alienda kama nani na kufanya nini?akasisitiza aache tabia ya kujipendekeza kwa mabalozi kitu kitakachopunguza confidence ya kutete maslahi ya nchi. N.B:kwa habari za wenyewe,Bhanji ameonekana kama ni mtu asiyejielewa,amekuwa akitumia mtandao wa facebook kujadili mambo ya ajabu,amekuwa akitukana matusi ya nguoni kwa wale wanaompa changamoto kitu ambacho hakiendani na hadhi yake,na wengi wanakiri ni vile uchaguzi wa EALA ulitawaliwa na rushwa za kila namna lakn Bhanji asingepita...kuna mkakati wa kumweka chini kumrekebisha.
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo shemeji yangu lol....:happy:
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Chadema ni mkufunzi mkuu katika nchi hii, pamoja na kuwa chama cha upinzani kwa sasa lakini ilani yao ya uchaguzi ndiyo inayotekelezwa, na mfumo wao wa kidemokrasia kutetea haki ndio unaofuatwa. Wanaofahamu huyu mama Makinda alivyokomalia Chadema kutoka bungeni hawawezi kuamini leo awahimize wabunge wa Afrika Mashariki toka Tanzania watume mbinu za Chadema kushinikiza kutoburuzwa bungeni na wabunge wenzao.
   
 14. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,013
  Likes Received: 2,227
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio viongozi tulio nao Tanzania! Kuiga kila kitu. Itafika mahali waseme kumatch out ni sera yao, pia hata peoples power ni slogan ya Chama cha magamba. Wakati makamanda wakitoka nje vikao vya bunge la kuongozwa kibabe bila mwongozo huyu mama alisema wanaenda kunywa chai. Leo anawaagiza hawa watoke nje kupinga kuburuzwa au watoke wakanywe chai? Ccm kuweni creative.
   
 15. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Hapo tu ndipo huwa naona siasa ni ya wapumbavu wasio na akili, leo unasema jambo fulani then kesho yake tu unabadili maneno, upumbavu mkubwa.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Alichonishangaza sana huyu Makinda pale aliposema alioingia bungeni kwa mara ya kwanza alikaa kimya muda mrefu bila kuchangia hoja nadhani sababu ya kutojiamini na woga. Leo anashangaa vijana wapya kabisa wanavyoingia na nguvu bungeni kushinda vikongwe wanaopiga usingizi tu kusubiria posho za vikao,
   
 17. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Yule mama nahisi hawezi hata kuongea mbele za watoto wake ili kuwapa ushauri. Hivi kweli ana watoto?.
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huyo ndo Makinda bana, mama mwenye watoto 5 kila mtoto na babake
   
 19. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Weee.....ulisikia ile mbinu ya wabunge wa Ukraine! Juzi walichapana makonde mpaka wengine kwenda kulazwa. Chezea politics wewe.....!
   
 20. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  mnyisanzu, hii sasa kali. ni kweli hii?

  wanaume watano (registered) walipita hapo. je wapembeni itakuwa wangapi!
   
Loading...