Makinda ukipinga hoja ya Zitto kishabiki unajiweka rehani subiri zamu yako; una hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda ukipinga hoja ya Zitto kishabiki unajiweka rehani subiri zamu yako; una hatari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Erasto..sichila, Apr 22, 2012.

 1. E

  Erasto..sichila Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makinda spika wa bunge letu ni spika asiye elewa wakati wote hisia za wananchi yeye maamuzi yake mengi huwa ni jinsi anavyo hisi basi ,tafakuri kwake no daima ni mama wa kupinga hata hisia za wananchi anaposhindwa kabisa hupenda kuonyesha hisia zake kuanza kufoka na hata kujisahau akatukana namuomba aelewa hicho cheo sio chake ni cha watanzania na asipo angalia atakuwa spika wa ovyo tangia uhuru atajitengenezea Cv chafu ya uongozi wa bunge hivyo namushauri apitishe hoja ya zito hiyo asubuhi ameshindwa muda wa ratiba apange ratiba ya hoja hiyo ninacho fahamu kwa upeo wake ataanza kufoka ovyo kisingizio muda hakuna na anamupa muda waziri mkuu atoe hotuba ya kufunga bunge mengine ukweli tunaombwe la uongozi wa bunge 'vaccum'yaani tabu hatutapata utendaji bora hata kidogo 'twafwa'
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yote uliyosema spika Anna Makinda hayajali, wa msingi kwake ni waliomuweka pale.
   
 3. j

  jjjj Senior Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakika hata mimi naliona hilo Makinda alionekana kuanza kupinga hoja kuwa imekiuka
  utaratibu na ni batili kwakuwa hajafikishiwa rasmi,sasa wewe unawezaje kujadili kitu ambacho hujaletewa na kuanza kukitolea maamuzi hata kukufikia mezani kwako hakijafika,Zitto mheshimiwa Mbunge amesema atawasilisha hilo swala
  jumatatu hujaona kilichomo ndani ya bahasha umesha sema nibatili.
  sasa basi muelewe haya mambo yalipofika sasa si ya wabunge peke yao sasa sisi wananchi tunaomba tukajiunge na Wabunge wetu kama wao mmeshindwa kuwasikiliza Dodoma,Basi sisi tunataka tuingie barabarani kwenye mikoa yetu
  tuliko kuomba uongozi wote wenye kashfa wajiengue maramoja.BETTER DIE THAN LIVE LIKE THIS WHILE FEW ENJOYS OUR TAXES.Wadau tunaomba muongozo namna ya kuanza jambo hili hapo jumatatu.
   
 4. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Tumpongeze Zitto-CDM kwa hatua ya uthubutu..hizi ndizo hisia za ujasiri tuzitakazo ila Mama Makinda nadhani ataipotezea tuu.Lamsingi hapa ni kuhakikisha wananchi wanafahamu madudu yanayofanyika ndani ya Bunge kwa mbinyo wa CCM
   
 5. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Let us wait 2morrow is not far
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Mama huyu ana jazba na kufanya mambo kama mwalimu wa shule yqa msingi. Kila kitu anataka mtoto akaombe ruhusa kwanza tena kwake. No independent thinking.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ashaanza kulipinga na kuliita batili tangia juzi ijumaa baada ya BBC kuripoti akiwa analiongelea!
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  nikisema kawekwa pale kwa kama kibaraka wa mafisadi ntakuwa nimekosea?
   
 9. E

  Erasto..sichila Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama spika ndiye mchawi wa maendeleo ya tanzania yaani haimuumi watu wamekwiba anawatetea kwa mizengwe sasa kesho mwacheni apinge hiyo hoja ila namuomba palepale akipinga basi mweshimiwa mmoja anyanyuke na kuomba muongoza kwa spika na atoe hoja yakutokuwa na imani na spika aombe yeye apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye hapo ndio akili itamukaa sawa vinginevyo kilasiku ni hayohayo yaani watanzania tunageuzwa mazuzu kila uchao watu wanaiba halafu wanaachiwa huru utakuwa wendawazimu ,napendekeza mbunge mmoja atoe hoja huyu mama ang'oke iwe kwisha habari yake 'kaul i mbiuTanzania kwanza Makinda baadaye
   
 10. N

  Negongo Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 25
  Nakuunga mkono kabisa,kwani huyu spika wetu anaonekana kabisa kupinga kila jambo jema linaloletwa na wapinzani,hili la kutokuwa na imani na mawaziri wazembe ni jambo la kitaifa wala sio la wapinzani,lakini yeye halioni hilo,huyu ni kumpiga chini tu!
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Nilizungumza jambo hili hapo kabla na hapa nitarudia! Let’s not try to undermine this old woman….tutake tusitake huyu mama anajua anachokifanya! Uzoefu mkubwa ndani ya bunge unamfanya awe conversant na sheria na kanuni kadhaa za bunge! Huyu mama, kanuni nyingi zipo kwenye her finger tips! Hutaki, unaacha! Tatizo la huyu mama si Umakinda wake, bali ndo tatizo la akina mama wengi! Kwa wale madereva, wanafahamu hili vizuri sana! Ukiwa barabarani, ni heri ukamatwe na Trafiki wa kiume kuliko wa kike! Hawa watu hawana dogo; wanasimamia sana misingi na wata-sticky hapo hata kama wakati mwingine busara ingelazimisha kuivunja misingi hiyo!

  Ningependa kukirudia nilichokisema awali:

  "Ni jambo lililo wazi kwamba watu hukosa haki zao kwa kutofahamu sharia! Aidha, mara kwa mara hoja zenye maslahi kwa taifa zimekuwa zikigonga mwamba bungeni kwavile tu baadhi ya wabunge wetu huwa wanakosa ufahamu wa sheria au kanuni za bunge! Kwa bahati mbaya, huku mitaani wengi wetu si wajuvi wa sheria wala kanuni za bunge na badala yake tumekuwa kama bendera zinazofuta upepo!

  Hoja ya Zitto Kabwe, juu ya saini 70 kwa ajili ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu naiunga mkono kwa 100%! Ni jambo lililo wazi kwamba, Waziri Mkuu pamoja na mawaziri wake wameshindwa kazi. Busara na uungwana wa siasa za kidemokrasia ni wao kuachia ngazi kwavile kilichotokea si majungu bali ni matokeo ya ripoti halali toka kwa taasisi za serikali zilizoainisha uozo na ufisadi serikalini. Kwa bahati mbaya, inaonekana kwamba Kanuni za Bunge haziruhusu kufanyika kwa Vote of No Confidence kwa sasa! Spika wa Bunge, amefafanua hili!

  Hapa, tuweke siasa za vyama pembeni na kuangalia maslahi ya taifa! Wapo watakaomponda Spika lakini yeye alichofanya ni kuangalia kanuni zinasemaje. Ni matumaini yangu Zitto Kabwe hakutoa pendekezo hilo kwa ajili ya kutafuta cheap popurality ya kisiasa!

  Hivyo basi, ikiwa Zitto alitoa pendekezo hilo kwa ajili ya maslahi ya taifa, basi aweke siasa pembeni na kufuata kanuni zinasemaje. Zitto na CHADEMA wasije wakarudi nyuma kutokana na kanuni kutoruhusu na kuamua kutumia mwanya huo kutangaza kwamba Spika na CCM wamekwamisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ili kumlinda. Kikao kijacho cha bunge hakipo mbali unless kama ipo namna ya kuitisha kikao cha dharura kushughulikia suala hilo. Hapa, ningependa kutoa wito kwa Zitto Kabwe na wengine wote (wabunge) wenye nia ya kweli ya kutokomeza ufisadi nchini kwamba wapigane kufa ama kupona kuhakikisha hoja inafikishwa bungeni kwenye kikao kijacho. Hapa, siasa ya vyama iwekwe pembeni na kuangalia maslahi ya Taifa. Ikiwa CHADEMA watataka kuitumia hoja hii kwa maslahi ya kisiasa basi hakika malengo yake hayatakuwa na manufaa yoyote kwa wananchi. Kuitumia hoja hii kisiasa itawafanya wabunge wa CCM kutounga mkono kwa vile wataona ni kuipaisha CHADEMA. Hata kama CHADEMA watazunguka dunia mzima kuelezea kukwamishwa kwa mpango huo, bado halitakuwa jambo lenye mbolea kwa maslahi ya taifa. Naamini, wapo viongozi wa CHADEMA na mashabiki wao ambao wangependa kuona CCM wanaikwamisha kura hii ili wapate sababu ya kushitakia kwa wananchi.Mawazo hayo hayana msingi na wala maslahi kwa taifa.

  USHAURI WANGU: Watokee wabunge wa CCM wasio na woga na walio tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio chama. Wabunge hao wajiunge na wabunge wa upinzani (kuunda kamati isiyo rasmi) katika kutafuta uungwaji mkono toka kwa wabunge wenzao ili kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ifanyike kwa mujibu wa sharia na kanuni za bunge! Pakiwepo na kamati ya aina hii isiyo rasmi, basi ile sura ya kisiasa itaondoka na hivyo kufanikisha zoezi zima la kuuwajibisha uongozi ulioshindwa."


  Hivyo basi, ikiwa pana nia ya dhati ya kufanya jambo hili kwa ufanisi na kuleta positive results, basi hapana budi Mheshimiwa Zitto afuate kanuni za bunge zinasemaje! Akiacha kufanya hivi, hoja itapigwa chini na hapo wa kulaumiwa sio Spika wa Bunge bali ni Zitto mwenyewe kwa kufanya jambo kinyume na taratibu.....sina shaka yoyote kama atafanya hivyo basi atakuwa amefanya makusudi.....ama kwa maslahi ya chama chake au kwa maslahi ya CCM! Anaweza ku-opt kufanya hivyo kwa makusudi kwavile anafahamu fika Watanzania wengi hatuatilii mambo. Hivyo, anaweza kwenda kinyume na kisha hoja kupigwa chini! Kwavile serikali haina kitengo cha proganda na kile cha CCM is dead; basi CHADEMA wanaweza kutumia mwanya huo kueneza propaganda kwamba serikali, spika na kwa kushirikiana na CCM wamezima hoja ya kuuwajibisha uongozi mbovu ulituhumiwa kufuja mabilioni ya Watanzania! Propaganda hii haitakuwa na maslahi kwa taifa hata kidogo!
   
Loading...