Wabunge kuwasilisha hoja kutokuwa na imani na Makinda - Ajali ya meli

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Anne.jpg

Ajali Ya Boti Yamletea Kasheshe Spika Wa Bunge

AJALI ya kuzama kwa Boti mali ya kampuni ya Seagull July 18, 2012 ilizua hali ya kwanini ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kukataa hoja ya kutaka kujadili suala la ajali hadi pale taarifa kamili zitakapotolewa hivyo mjadala wa Bajeti ya Wizara ya mambo ya Ndani uendelee.


Kutokana na ajali hiyo, muda mfupi baada ya kipindi cha jioni kuanza, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisimama na kuomba mwongozo kwa kutumia Kanuni ya 47(3) kulitaka Bunge lipitishe Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mafungu bila ya kutolewa ufafanuzi ili wabunge waweze kupata muda wa kujadili tukio hilo.


Hata hivyo, Spika Anne Makinda alipinga hoja ya Hamad na kutaka Bunge liendelee akieleza kwamba kanuni hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na kwamba tayari ameshawasiliana na waziri husika na kwamba taarifa kamili zitakapopatikana angelitaarifu Bunge.


Baada ya kauli hiyo Spika Makinda aliruhusu shughuli za Bunge ziendelee na kumwita Silima kutoa ufafanuzi wa hoja za wabunge.

Lakini wakati Naibu Waziri huyo akielekea kutoa hotuba yake, wabunge wote wa CUF, Chadema na baadhi wa CCM walitoka nje na kwenda katika Ukumbi wa Msekwa ili kupeana taarifa za ajali hiyo na kupanga mikakati ya jinsi ya kutuma ujumbe wa haraka kwenda Zanzibar kushirikiana na waokoaji.
Ukumbi huo uligeuka kuwa wa maombolezo kwa muda baada ya wabunge wengi kuangua vilio pale walipopewa taarifa rasmi za ajali hiyo.


Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid alieleza kwa ufupi tukio lilivyo na kwamba wangemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda awasaidie ndege ya Serikali ili waweze kwenda Zanzibar kujumuika na wenzao katika tukio hilo.


Baada ya Hamad kumaliza alisimama Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia ambaye alijaribu kuwatuliza wabunge akisema kuwa, meli inaweza kuzama lakini watu wasipoteze maisha kutokana na kuchukua muda, kauli ambayo ilipingwa na wabunge wengi.
Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Ibrahim Sanya alimshutumu Spika Makinda akisema, amekosa hisia na hajui kwamba kuzama kwa meli ni janga la kitaifa.
“Kwa hili hata nikikutana na Spika nitamwambia kweli ameniudhi. Sihitaji ubunge kama hali yenyewe ndiyo hii na tutapiga kura ya kutokuwa na imani na Spika,” alisema Sanya.


Wakati hayo yakitokea, katika Viwanja vya Bunge baadhi ya wabunge na mawaziri walionekana wakiwa katika vikundi wakijadili suala hilo, huku wengine wakipinga uamuzi huo wa Spika.


Wakati hayo yakiendelea katika Ukumbi wa Msekwa, Bunge lilikuwa likiendelea kumsikiliza Silima akijibu hoja za wabunge na baada ya kumaliza, Spika Makinda alimwita mtoa hoja, Waziri Nchimbi naye kujibu.
Lakini badala yake, alitumia fursa yake kuondoa hoja ya Makadirio ya Matumizi ya wizara yake ili kutoa fursa kwa Bunge kujadili ushiriki wake katika tukio la kuzama kwa boti hiyo.


Dk Nchimbi alitumia Kanuni ya 58 (5) ambayo inamtaka mtoa hoja kusimama na kutoa hoja ya kuondoa mezani hoja yake kama kuna jambo la dharura.


“Mheshimiwa Spika, natumia Kanuni ya 58 (5) ambayo inamtaka Waziri kusimama na kutoa hoja ya kuondoa mezani hoja yake kama kuna jambo la dharura,” alisema Dk Nchimbi.


Dk Nchimbi aliendelea: “Ikumbukwe Mheshimiwa Spika, muda mfupi kabla ya kuingia hapa ndani uliniita mimi na Naibu Waziri ukataka tukueleze hali ya ajali hiyo na kwa wakati huo Kamishna wa Matukio Zanzibar alikuwa eneo la tukio. Sasa basi, kutokana na agizo lako, ni imani yangu kwa muda aliotumia Naibu Waziri unatosha kuendelea kufuatilia jambo hilo.”


Baada ya kutoa maelezo hayo, Wabunge wote 49 waliokuwa wamebaki katika ukumbi walisimama kuunga mkono hoja.


Baada ya hapo, Spika Makinda aliwahoji na kwa kauli moja waliridhia kuahirishwa kwa kikao hicho wakati huo ikiwa saa 11:31 hadi leo saa 3.00 asubuhi, huku akiitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya Bunge jana hiyohiyo kujadili suala hilo.


Akizungumza baada ya kikao hicho cha Kamati ya Uongozi, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema, limeamua kufuta kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu na kwamba kikao cha Bunge kitaendelea leo asubuhi kuanzia saa 2:00 kupokea taarifa ya Serikali kisha watajadili mustakabali wa vikao vya Bunge.Kamati hiyo pia iliamua kutuma ujumbe wa wabunge kwenda Zanzibar kuwafarijiwa wale wote walioathiriwa na ajali hiyo.


Imeandikwa na Salma Said, Zanzibar, Neville Meena, Habel Chidawali na Boniface Meena, Dodoma; Raymond Kaminyoge, Aidan Mhando, Dar es Salaam.
 
Kwa hili Mh. Spika Makinda inabidi awajibishwe!..

Kulikuwa na kila dalili ya mama huyu kujisahau na kutumia jazba kwenye handling ya mambo ya msingi kabisa toka mwanzo. Sishangai kama sasa hivi ameingia kwenye kaburi alilokuwa analichimba mwenyewe. Ukali unafaa nyumbani...huku kwenye watu wa aina zote, lazima hekima itumike ili mambo yaweze kwenda.
 
Kulikuwa na kila dalili ya mama huyu kujisahau na kutumia jazba kwenye handling ya mambo ya msingi kabisa toka mwanzo. Sishangai kama sasa hivi ameingia kwenye kaburi alilokuwa analichimba mwenyewe. Ukali unafaa nyumbani...huku kwenye watu wa aina zote, lazima hekima itumike ili mambo yaweze kwenda.
Sasa naipata picha vizuri kuna mtu alianzisha mada kama hii akisema Hamad Rashid alitaka bunge liahirishwe kwa sababu ya msiba kumbe alitaka bunge lijadili ajali hii na Makinda akakataa.. Unaona jinsi taarifa moja inavyoweza kutuvuruga... Ila nashukuru kwamba msimamo wangu hautabadilika. Nilikuwa radhi kuwalaumu wabunge wa Upinzani kumbe maskini walichokitaka ndicho nachokisimamia..
 
Tatizo la viongozi kutanguliza mamlaka waliyo nayo kama kinga ya kazi yao wakati wanatakiwa kuangalia unyeti wa jambo la dharura. Majuzi tu aliacha kikao Dodoma kwenda kwenye msiba wa mtu aliye wa karibu naye, lakini inapokuja msiba wa kitaifa na yeye akiwa kama mmoja wa mhimili wa serikali kuonyesha dharura hiyo, yeye anadharau na kuwekea ngumu uamuzi wa wabunge walio wengi kwa kupindisha kanuni.

Hata pale alipobakiwa na wabunge 49 tu baada ya wengi wa wabunge wa upinzani na wa ccm kuondoka kwenda kufanya kikao chao cha dharura ukumbi wa Msekwa, lakini Makinda bado alikuwa na kichwa nguvu hadi pale Waziri Nchimbi alipoamua kwa hiari yake kuokoa jahazi kwa kuondoa hoja ya bajeti mezani ili watu waende kushiriki tukio la msiba wa kitafia.

Hii ni dalili tosha kwamba Makinda Speaker wa bunge letu si mtu makini katika kuangalia mambo muhimu ya kitaifa na hana uwezo wa kupima uzito wa matukio ambayo yanatikisha taifa. Sishangai wabunge walioamua kutoka kwani uchungu walio nao ni tofauti na mama huyu alivyo na moyo mgumu.
 
Sasa naipata picha vizuri kuna mtu alianzisha mada kama hii akisema Hamad Rashid alitaka bunge liahirishwe kwa sababu ya msiba kumbe alitaka bunge lijadili ajali hii na Makinda akakataa.. Unaona jinsi taarifa moja inavyoweza kutuvuruga... Ila nashukuru kwamba msimamo wangu hautabadilika. Nilikuwa radhi kuwalaumu wabunge wa Upinzani kumbe maskini walichokitaka ndicho nachokisimamia..

Jambo hili ni la kawaida kabisa itokeapo dharura katika mabunge ya nchi nyingi, ajenda za kawaida husitishwa na kujadili dharura, na ulivyosema Mkandala hoja ilikuwa kujadili dharura ya kuzama meli si kuondoka bungeni. Kiburi cha Makinda kilifanya wabunge wamfanye jeuri ya kuondoka kwenda kufanya kikao chao kisicho rasmi na kiti cha Speaker, jambao ambalo kama ubongo wake unafanya kazi sawa sawa anajiona amefedheheshwa na kutakiwa kuliomba radhi bunge na watanzania.
 
Jambo hili ni la kawaida kabisa itokeapo dharura katika mabunge ya nchi nyingi, ajenda za kawaida husitishwa na kujadili dharura, na ulivyosema Mkandala hoja ilikuwa kujadili dharura ya kuzama meli si kuondoka bungeni. Kiburi cha Makinda kilifanya wabunge wamfanye jeuri ya kuondoka kwenda kufanya kikao chao kisicho rasmi na kiti cha Speaker, jambao ambalo kama ubongo wake unafanya kazi sawa sawa anajiona amefedheheshwa na kutakiwa kuliomba radhi bunge na watanzania.
Kuna watu hapa JF walitupotosha na kutuaminisha kwamba wabunge walitoka kwa sababu walitaka bunge livunjwe kwa ajili ya msiba.. Hii haikuniingia akilini kabisa ndio maana nilisimama na wale waliotaka bunge liendelee kujadili swala hili..Sasa nimeelewa vizuri na niko pamoja na Upinzani. By the way Mimi mkerewe unatumia R badala ya L kwenye mkandara ahaa! ahaha!
 
Hiki ni kiburi kisichokua na mfano. Amezoea kuklisha wenzakke wakati wanatoa hoja xza busara na wengine kuwatoa nje ya bunge safari hii inakula kwake. Ajali illiyotokea ni ajali ya kitaifa na waliokua wanaomba kuhairishwa kwa bunge ni kwenda kuungana na wapiga kura wao. Kwa upande wa pili cuf wajifunze kuwa huyu mama hamnazo anapopambana na wabunge wa cdm alafu wao wanakaa wakichekelea. Haiingii akilini kwa mama mwnye umri kama wake na asiweze kuishi au kuwa na mume lzm ana ksoro. Huwezi kuwa na sura mbaya kama unapiga vigelgele msibani alafu utarajie kuwa na maamuzi ya busara. Analoa na safari hii atajuta kuumbwa wa kike.. nyamafu
 
Kuna watu hapa JF walitupotosha na kutuaminisha kwamba wabunge walitoka kwa sababu walitaka bunge livunjwe kwa ajili ya msiba.. Hii haikuniingia akilini kabisa ndio maana nilisimama na wale waliotaka bunge liendelee kujadili swala hili..Sasa nimeelewa vizuri na niko pamoja na Upinzani.

Tatizo wengi wetu huleta mada ambazo hazijawa published na vyombo husika to the public audience, na pengine huzisikia kwenye vyombo vingine vya habari na hivyo kutofuatilia kwa makini nini hasa kimezungumzwa, na matokeo yake wanaposti kitu ambacho ni kinyume kabisa na kilichotamkwa. Tupo wengi tusio na subira ya kutaka kupata habari kwa uhakika au kuhakiki habari iliyopo.

Tusishangae hilo Mkandala, ujuavyo JF inakusanya wengi akiwemo Mkandala, Candid na wengineo, kwa maana hiyo tufauti ya post na namna tunavyozichukulia mada na ukweli au hali halisi inategemea ni nani anayeleta kwani Mkandala ataleta kwa kiwango na uelewa wa Mkandala, na Candid hali kadhalika. Samahani kwa ufafanuzi huo.
 
Poleni wote m/walofikwa na msiba huu. Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amina
 
Sioni hilo likitokea katika bunge lililojaa watu waoga wa kufanya maamuzi magumu!!!!
 
Tena mkuu? kwenye thread ile nyengine umetetea aliyoyafanya,,hapa tena unamkaanga?
Kwa sababu kule alilaumiwa Makinda kwa kutoahirisha bunge kwa sababu ya msiba lakini hapa inaonyesha haikuwa kuahirisha bunge isipokuwa kuzungumzia janga lilotokea..

Sasa tazama, mimi msimamo wangu haujabadilika yaani nilitaka bunge lizungumzie swala hili kutafuta ufumbuzi wa janga lilotokea lakini wale waliokubali bunge liahirishwe kwa sababu ya msiba wakisoma hapa watashindwa kukaa upande maana wabunge wa upinzani hawakutaka bunge liahirishwe wakati wao wanatetea bunge kuahirishwa..
Je, wamesimama wapi sasa?
 
Tena mkuu? kwenye thread ile nyengine umetetea aliyoyafanya,,hapa tena unamkaanga?

Ndugu yangu tatizo ni mada ilivyowasilishwa, na baada ya kuangalia ukweli mada haikuwasilishwa kama ilivyotukia bungeni. Hakukuwa na sababu ya kusimamisha kikao cha bunge, watoke waende wapi? Kuna ajali ya moto ndani ya jengo la Bunge? Hata kama kungetokea ajali kama hiyo basi wangetoka nje ya ukumbi na kukusanyika sehemu ili kupata nafasi ya kutuliza akili na kupata maelekezo nini cha kufanya.

Bunge lilitakiwa kujadili tukio hilo, na kwa walipo wengi wenye busara neno la maana lingetokea na kwa vyo vyote wangeamua kutuma ujumbe kwenye dharura, si wabunge wote waende dharurani. Makinda alikosa busara, na wabunge waliotoka bungeni uzalindo uliwasukuma kufanya hivyo.
 
Anna makinda ana sumbuliwa na nini mpaka ana kosa utu kiasi hiki?

Sidhani kama alifikiri kwa kina.
 
Anna makinda ana sumbuliwa na nini mpaka ana kosa utu kiasi hiki?

Sidhani kama alifikiri kwa kina.

Tatizo la pekee ukimsoma ni ile saikolojia ya kujiona ana mamlaka ya mwisho pale mjengoni, na kuendekeza hilo hujengekea kale katabia ka kudharau hata mambo makubwa hata mtoto mdogo akashangaa. Watu wa aina hiyo hupenda jambo la muhimu litoke katika vichwa vyao, kwani kukubaliana na yatokeayo kwa vichwa vya wengine ni kuwadhalilisha kwamba hawafikiri kutosha. Lakni kwa wenye kujali taadhima ya utumishi wao kwa umma na watu anaowatumikia ni heshima kujali hoja za anaowatumikia kwani yeye ni kiongozi na wala si mtawala. Makinda anaakisi kama mtawala - mtwa. Kiongozi huunganisha hoja za walio chini yake na kuzifanyia kazi si kuzipinga.
 
Back
Top Bottom