Makinda awa Rais mpya Bunge la SADC

Makinda awa Rais mpya Bunge la SADC

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
anna4makinda.jpg

MKUTANO wa 36 wa Bunge la nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), umemchagua kwa kishindo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuwa Rais wa Bunge hilo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mbunge wa Malawi, Njovya Lema amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais. Makinda, ambaye hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, aliungwa mkono na wajumbe wote wa mkutano huo, ambao ni Maspika na Wabunge kutoka mabunge ya nchi wanachama wa SADC.

Alichaguliwa wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 36 wa Jukwaa la Mabunge ya SADC, uliokuwa ukifanyika mjini hapa.

Msimamizi wa uchaguzi, ambaye ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC, Dk Esau Chiviya alisema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za Bunge hilo, Kanuni ya 42 (2) inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na mgombea mmoja pekee, basi atawahoji wajumbe na endapo watamkubali basi atamtangaza rasmi kuwa amechaguliwa kushika nafasi hiyo.

"Kwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda hana mpinzani na kwa kuwa nimewahoji na wote mmemuunga mkono, basi natangaza kuwa ndiye Rais mpya wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo," alitangaza Dk Chiviya.

Awali, kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi ndani ya chombo hicho, Makinda alitakiwa kugombea nafasi hiyo pamoja na Spika wa Ushelisheli na Msumbiji, ambao hawakushiriki uchaguzi huo na badala yake walimuunga mkono Makinda.

Akisoma hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Mkutano huo, Makinda alisema: "Ninalo deni kubwa kwenu kwa jinsi mlivyoniunga mkono na kama mnavyojua jukumu letu kubwa mbele yetu ni kuwa na Bunge imara la SADC, jambo ambalo nawahakikishia kwa pamoja tutafanikiwa.

"Kama mnavyojua, malengo makuu ya SADC PF ni kuwa na Bunge la kikanda litakalowakilisha mawazo ya pamoja kutoka kila Bunge la Nchi wanachama wa SADC, hili ndilo lengo kuu la waasisi wa umoja huu walilokusudia wakati wa kuanzisha chombo hiki mwaka 1997 hivyo na sisi lazima tulienzi na kulitekeleza."

CHANZO: Habari Leo
 
Congrats mama - Katuwakilishe vizuri
Ushauri -Ongeza confidence haswa kwenye kidhungu
 
Ataongeza tija gani kwa Tanzania?

Tuna bunge la EA lakini wananchi wa kawaida hatuoni manufaa ya chombo hicho zaidi ya kusikia wabunge wa Tanzania wakituaibisha tu.

Kila rakheli, ila asije kuwa kama
Shy-rose.
 
inatusaidia nini sie walala hoi?
 
Congrats mama - Katuwakilishe vizuri
Ushauri -Ongeza confidence haswa kwenye kidhungu

kashindwa kuwakilisha bunge la taifa huko anaenda picnic tu aende asiende hatupati chochote
 
Lakini mama huku Tanzania watoto zako wakina makonda wanawapiga babu zao wakina WARIOBA
 
hongera. wenye wivu kajinyongeni. na mimi nasema kajinyongeni tu.
 
wamemchagua kwa sifa gani au wanaangalia sura
 
Ataongeza tija gani kwa Tanzania?

Tuna bunge la EA lakini wananchi wa kawaida hatuoni manufaa ya chombo hicho zaidi ya kusikia wabunge wa Tanzania wakituaibisha tu.

Kila rakheli, ila asije kuwa kama
Shy-rose.

Ww nafkiri sio Mtanzania, na kama ni Mtanzania ndio wale jobless sababu siamin kama uliomba kazi kupitia vyeti vako.
Ushawahi kuona neno "rakheli" uf@l@ mkubwa kwa kweli!
 
Back
Top Bottom