Makinda ampinga Zitto hoja ya Kumuondoa Waziri Mkuu

Bi Kiroboto amefanya hivyo kwa maslahi binafsi. Maslahi ya chama!!! Nafikiri kwanza hawakuamini kuwa sahihi zitatosha ... maana wangekuwa wametoa kauli hiyo toka asubuhi. Lakini wameona zimefika 66 wanajua inawezekana sasa wanataka wawaaminishe watz kuwa Zitto kakosea.
Mkuu mtendee haki spika haitwi BI KIROBOTO, muwe na heshima kwa watu wazima bana.
 
Mkuu soma katiba Ibara ya 53A na ibara ya 42. Hapo utapat utaratibu wa kikatiba jinsi ya kupiga kura ya kutokuwa na imani n PM.

Shida ya Tanzania ya sasa ya magamba, kitu kimoja kinakuwa na kanuni mbalimbali, sheria kibao, so inakuwa ni vigumu sana kutekeleza mambo, naona suruhu itakuwa kwenye katiba mpya.
 
wana jf spika makinda amekataa hoja ya kumpiga chini pm. sababu hapa imekuwa ni siku zinatakiwa ziwe si chini ya 14, sasa leo wameshapata sahii zote lakini siku 14 hawawez kufikisha bunge linaisha j3 na hvyo tutakuwa na siku 4 tu.
nawasilisha


Mkuu hujasoma katiba na kanuni za bunge? Hajaikataa ila anachokifanya Zitto ni process ambayo inafaata mahitaji ya katiba na kanuni za bunge. Kitu cha kwanza kabisa ni kuwa na asilimia 20 ya wanaounga mkono hoja hiyo ili kuiwakilisha kwa spika kwa maandishi. Hiki ndicho Zitto anafanya ili apate 20% and then apeleke hoja hiyo kwa Spika ndani ya siku 14 baada ya kutoa kusudio la kuiwakilisha. Spika anachosema eti zoezi ni batiri anajaribu kuwa discourage wabunge mbumbumbu wasiweke sahihii zao wakidhani zoezi halitakiwi.

Hoja hii inaweza kuwakilishwa hata bunge lijalo kwani isingekuwa rahisi kutimiza masharti ya siku 14 maana bunge linaisha jumatatu.

PM ndo atendelea kupandwa na pressure tu maana jambo hili litakuwa linamsubiria mpaka mwezi wa sita wa bunge lijalo ni bora hata ingefanyika sasa ilikumshusha pressure. Atatakiwa achague moja kati ya haya mawili. 1. kuwapiga chini hao mawaziri watuhumiwa. 2. Au asubiri kusurubiwa kwenye bunge la mwezi wa sita.
 
kwa wale wataalamu wa mambo ya sheria na kanuni za bunge, naomba kuelimishwa,
Hivi zito anaweza kuwasilisha hoja j3, then baada ya wiki 2 (siku 14) spika akitisha kikao cha bunge kwa ajili ya kupiga kura za siri? inawezekana?
Nielewewavyo mimi, Siku 14 baada ya kuwasilishwa kwa Hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni minimum number of days lkn spika anweza kuitisha bunge la dharura ila hata fanya hivyo sababu haitakuwa kwa maslahi ya chama tawala na serikali. Sahihi zitaenedelea kukusanya na hoja itajadiliwa hata bunge lijalo. Hatimaye mbunge litachukua hatua stahiki. Tuwe wavumilivu; mwisho wa magamba u-karibu.
 
wabunge wazalendo tieni tu sahihi zenu zikifika hizo 70 ili hiyo hoja ije ijadiliwe bunge lijalo siyo mbaya bado miezi miwili tu.
 
Mlitegemea nini kutoka kwa kada wa CCM. Hawa wote wanafanana. Tofauti yao ni pale wanapovizia mwenzake aondoelewe ili yeye aingie, nothing more. Kuna makanda wachache sasa wapo CCM wanapiga right timing ili waruke upande mwingine. certainly JM is not one of these!
 
Wakuu nani ana katiba karibu a paste hapa hiki ibara ya 52 ambayo ndiyo labda spika anweza kuitumia kuzuia hii move. Ibara hii inaongelea kazi za PM. Maana ili awajibishwe na bunge lazima tuhuma ziwe na uhusiano na kazi za PM ambazo ziko kwenye ibara hii ya 52.
 
Siku zizizopungua 14, kabla ya siku inayokusudiwa kufikishwa. Hapa hakuna shida wala haraka. Hoja itasubiri tu na haitaoza. Hazijatajwa siku zinazozidi. Hii itakuwa Ni kwa faida ya mawaziri kuwa na muda mzuri wa kujihoji wajitoe au wamtose waziri mkuu. Mazuri hayataki haraka. Bado pia haizuii kujipanga upya.
 
anafurahia kusafiri kwenda norway kujifunza eti namna ya kutumia mafuta na gesi hapo kesho
wao ni mainjinia wa hayo mambo? kwanini hiyo kazi wasipewe watu wa TPDC kwenda kuangalia?
hana uchungu na nchi
kanuni zitarekebishwa tu wabunge watakaa hata kwa dharura
lazima wazirir mkuu angoke
uyu dogo naye sio kabisa... yaani uanajiri housegirl then unaenda wewe kujifunza kupika...
halafu nini kitokee.....
 
Mwanasiasa kijana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) amewataka watanzania wasichanganyikiwe kufuatia kauli iliyotolewa na January Makamba na mwongozo uliotolewa na Spika Anne Makinda kwani wanajua wanachokifanya na wanafuata kanuni za bunge na sheria za nchi yetu (katiba) kama zinavyotaka, ili kukidhi matakwa ya kupeleka hoja ya KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU.

Na ni vyema ikaeleweka kuwa lengo la HOJA HII si kutafuta maarufu kama January Makamba anavyotaka ieleweke bali ni kulinda misingi ya kidemokrasia ya UWAJIBIKAJI na USIMAMIZI wa Serikali unaopaswa kifanywa na Bunge.

Tunataka bunge litoke kwenye Ulalamikaji mpaka kwenye Utendaji
 
Wadau naomba ufafanuzi kwa mwenye kujua sheria za VOTE OF NO CONFIDENCE! Sheria inahitaji asilimia ngapi ya wabunge ili kuleta hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu! Kura pia inahitaji asilimia ngapi ya Wabunge ili PM apigwe chini? Kura 70 ni asilimia ngapi ya wabunge?



Wana JF
Tafadhali, someni kwa makini na muelewe kanuni za bunge zinasemaje kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu na taratibu zake

SEHEMU YA KUMI NA TATU (ya kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007)
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU

133.-(1) Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa
Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
kwa mujibu wa Ibara ya 53A ya Katiba.

(2) Hoja yoyote ya kutaka kupitisha Azimio la kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu haitatolewa Bungeni endapo:-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya
Waziri Mkuu yaliyoainishwa katika Ibara ya 52 ya
Katiba;

(b) hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(c) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa; au

(d) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa
kuipitisha.

(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa
na Bunge isipokuwa tu kama:-

(a) taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na
kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua
asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa
kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne
kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;

(b) Spika ataridhika kuwa masharti ya Katiba kwa
ajili ya kuleta hoja hiyo yametimizwa.

(4) Hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya
Katiba, itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na
itaamuliwa kwa kura za siri.

(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo
inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

(6) Endapo hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa
na Bunge kwa kupigiwa kura na Wabunge walio wengi, Spika
atawasilisha Azimio hilo kwa Rais na mapema iwezekanavyo na
kwa vyovyote vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha
Azimio hilo, Waziri mkuu atajiuzulu na Rais atamteua mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu



hakijaharibika kitu huu ni mtego mkubwa kwa serikali ya CCM waende wakavue gamba kiukweli, Bunge la bajeti likikaa kama gamba bado litaendelea kuwepo Mh.Pinda kwaheri maana tayari sahihi za kummg'oa zipo
 
ukombozi haiutaletwa kwenye sahani kama pilau .....lazima mizengwe itakuwepo kwa hiyo ...... kwa hiyo Zitto kaza buti kuna vipengele vingine vya dharura vinatengua hiyo kanuni, muhimu saini 71 zipatikane.
Wakishapata hizo na hoja ikienda bungeni hili kumuondoa Pinda kunaitajika kura kama 100 za wanaCCM plus wapinzani wote.Kazi ni ngumu hapo.
 
Wakuu nani ana katiba karibu a paste hapa hiki ibara ya 52 ambayo ndiyo labda spika anweza kuitumia kuzuia hii move. Ibara hii inaongelea kazi za PM. Maana ili awajibishwe na bunge lazima tuhuma ziwe na uhusiano na kazi za PM ambazo ziko kwenye ibara hii ya 52.
Usiwe mvivu nenda jukwaa la katiba mpya utaikuta kule!
 
Ni mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali. Hii ni pamoja na kuteua mawaziri kwa kushirikiana na mh rais
 
Mie naona mbio za CCM kuimbia chadema zimefikia hapa
kuku.jpg
hata wafanyaje, wataliwa tu

Akina January wanajaribu ku-equal Zitto's intelligence kitu ambacho hakiwezekani

January comes from a silver spoon and Zitto ni mtoto wa kikopo
 
Back
Top Bottom