Suala la wanaona kawaida ama la subiri wenye nayo waje,nachojua mimi mtu mwenye makengeza anawapa changamoto wasio nayo,mfano mjomba wangu(rip) alikuwa anaweza kuzungumza jambo halafu ukimtazama unaona macho yake yamekaza kuangalia mlangoni,unampotezea unaendelea na ishu zako lakini kumbe yeye alikuwa anakuangalia wewe!mwingine alikuwa ni mwalimu wangu wa primary alikuwa mkali balaa,akiwa class hataki hata mtu ajitikise,yeye alikuwa akitoa quiz basi anasimama dirishani anatazama nje,ila jicho lake la kushoto linatutazama sisi...kumbe hata hatuoni!basi tunakosa amani kabisa.