Makengeza ni kilema au ugonjwa?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,551
Kila mtu anafahamu makengeza.

Mtu kuwa na makengeza anatafsiriwa kama mgonjwa au ana kilema ?

Ukiwa na makengeza unaona kawaida au kuna changamoto yoyote ?

Nini hasara ya kuwa na makengeza kwenye uonaji ?

Nisiwachoshe.
 
Suala la wanaona kawaida ama la subiri wenye nayo waje,nachojua mimi mtu mwenye makengeza anawapa changamoto wasio nayo,mfano mjomba wangu(rip) alikuwa anaweza kuzungumza jambo halafu ukimtazama unaona macho yake yamekaza kuangalia mlangoni,unampotezea unaendelea na ishu zako lakini kumbe yeye alikuwa anakuangalia wewe!mwingine alikuwa ni mwalimu wangu wa primary alikuwa mkali balaa,akiwa class hataki hata mtu ajitikise,yeye alikuwa akitoa quiz basi anasimama dirishani anatazama nje,ila jicho lake la kushoto linatutazama sisi...kumbe hata hatuoni!basi tunakosa amani kabisa.
 
Duh nakumbuka nikiwa primary kuna teacher mmoja mmama alikua na kengeza unaweza kudhania anaangalia mtu mwingine kumbe anakuangalia wewe
 
Mtu mwenye makengeza huwa anaona kwa macho yote au ni jicho moja ndio limafanya kazi..
Kwamba Jicho moja linavyoangalia mashariki na jingine mangharibi yote yanapeleka image kwa usahihi au?
 
Mtu mwenye makengeza huwa anaona kwa macho yote au ni jicho moja ndio limafanya kazi..
Kwamba Jicho moja linavyoangalia mashariki na jingine mangharibi yote yanapeleka image kwa usahihi au?
 
Ukiwa na manzi mwenye makengeza raha sana,unaweza fanya tukio ukiamini kuwa hakuoni kumbe anakuona vzr sana!
 
Inasemekana MUHIMBILI wana hii huduma ya Strabismus surgery, kuna mtu ana uhakika juu ya hili?

Yaani namaanisha aliwahi kufanya upasuaji wa macho makengeza? Aliyenambia ni daktari wa MUHIMBILI ila sio daktari bingwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom