Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,157
- 4,457
Kwasababu hili jukwaa lina watu wenye kada/uzoefu/taarifa mbalimbali nadhani naweza kupata majibu. Binafsi nimekuwa najiuliza maswali mengi kuhusiana na makazi ya watu yaliyopo pale kunduchi karibu kabisa na jeshi eneo wanalochimba kokoto.
Kwanza ningependa kujua kama serikali inaruhusu watu kujenga makazi katika lile eneo
Jeshi limechukua tahadhari gani kuzuia yasije jitokeza yaliyotokea Mbagala na Gongolamboto maana wakazi wanaongezeka kwa kasi sana katika eneo lile.
Kama serikali hairuhusu watu kujenga makazi katika lile eneo, kwanini imewaacha watu wanaendelea kujenga nyumba za kisasa ambazo siku zikibomolewa ni hasara hata kwa Taifa.
Sheria za mikataba zinasema mkataba wowote unaoingiwa katika mazingira yaliyovunja sheria za nchi ni batiri, Kama lile eneo haliruhusiwi kujenga makazi. Je Tanesco inafanya biashara haramu na wakazi wa pale? Kwasababu Tanesco wamepeleka huduma za umeme eneo lile japo kuna tetesi kwamba siyo makazi halali ya raia.
Kuna kipindi milipuko ya baruti za kulipua kokoto husikika maeneo yale, serikali kwanini isiingile kati? maana ni kero kwa wakazi wa pale.