Makazi ya waathirika wa mafuriko

Bitabo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
1,900
687
Wana JF hebu tulijadili hili la waathirika wa mafuriko.Nimekuwa nafatilia taarifa za habari naona makampuni na watu binafsi wanajitolea kwa moyo kuwapa msaada wenzetu walioathiriwa na mafuriko. Ni swala jema na la kujivunia kwamba Watanzania bado tuna moyo wa kujitoa na kuwasaidia wenzetu. Kitengo cha maafa cha Mizengo Pinda ambaye yuko likizo nahisi nacho kiko likizo.
Sasa kwa swala la makazi, hata kama watapewa viwanja kama JK alivyosema, sidhani kama wana uwezo wa kujenga nyumba mpya.Maisha yao yameathiriwa sana kuanzia kisaikolojia mpaka kifedha.
Nadhani ule mpango wa NHC wa kujenga nyumba na kuwakopesha wananchi kwa kutumia mikopo maalum ya benki ndo ulitakiwa uanzie hapa. NHC ingejenga nyumba za bei nafuu then hawa watu wapangishwe na wasaidiwe kupata mikopo hiyo bank na serikali iwaguarantee.
Jamani kwa sisi wa kipato cha chini, nadhani mnajua ilivyo kazi kujenga nyumba. Mtu alishajikusanya mpaka akaweka kajumba kake japo ni bondeni lakini alikuwa anaishi vema na familia yake. Sasa mvua imepiga na vitu vimesombwa na Mungu bariki nyumba haijabomoka, unadhani mtu huyu atakubali kuhama ache kajumba kake akachukue uwanja mtupu huko kusikojulikana???
Hebu serikali yetu ingawa sio sikivu basi angalau kupitia kwa wana JF walio karibu na Baba Riz wamfikishie wazo hili. La sivyo tutaendelea kuona mafuriko kila mwaka mvua zikipiga.
Nawasilisha
 
Mh hapo mi napita tu....ila ingekuwa busara km serikali ingeliangalia hilo kwa ukaribu.
Wazo zuri
 
Wazo ni zuri tatizo ni kwa Jk na timu yake kwa sura ya ubinadamu walikwisha kuivua siku nyingi na sasa wamebaki kuwa watu tu
 
Back
Top Bottom