...Makavu Laivu..........!!!

...Makavu Laivu..........!!!

Kivumah

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Posts
2,427
Reaction score
1,061
Kwa Wadada:
Kwa dada zangu wote wa kizazi hiki chetu: Sababu zinazoweza kukufanya ukose mchumba ukabaki singo muda mrefu au maisha yote huku unalialia:

1. Kutokuwa na hofu ya Mungu. Binti huendi kanisani wala msikitini upo tu nyumbani. Mvulana serious akikuangalia ataona ni mtu wa kutumika tu na si mtu unayeweza kulea watoto katika misingi ya maana na kuwa muhimili wa familia.

2. Masaa 24 wewe uko kwenye simu na TV. Ukitoka channel hii unahamia ile. Tamthilia zote unazijua wewe. Hebu niambie kichwa chako kitakuwa kimejaa nini zaidi ya mapenzi ya Kifilipino na Kimeksiko ya kwenye hizo tamthlia?...


3. Hutaki kufanya majukumu ya msingi ya kike kama kupika na kuosha vyombo, kisa TV na sinema zimekuonyesha kuwa hayo pia ni majukumu ya wanaume. Hii ni Afrika mama, utaumia. Unaenda kwa mpenzi wako kumtembelea vyombo unakuta vichafu huoshi, unakaa tu. Unajishushia pointsi. Osha na mwambie si vizuri kuacha vyombo vichafu.!

4. Kuwa mtumwa wa kila kitu kipya. Mtu gani atapenda kuwa na mwanamke ambaye ni mtumwa wa kila aina mpya ya simu, kila aina mpya ya kiatu, kila aina mpya ya nguo, kila saluni mpya anataka kwenda?

5. Kutumia vipodozi hadi unapitiliza. Badala ya kuvutia unatisha!

6. Muda mwingi kutumia kwenye mitandao. Mara Twitter, Mara Facebook, mara Instagram! Wataalam wanasema binadamu ana uwezo wa kuwa na marafiki si chini ya 150 tu. Lakini wewe kila mtandao una watu 2,000! Sasa hivi unaweza kuona haina maana ila ngoja ufike miaka 35 ukiwa single and searching ndo utaelewa.


7. Acha kutoa namba yako kwa kila mwanaume! Hakuna mwanaume ambaye anataka kuwa na mwanamke ambaye kila muda anawasiliana na watu hata wasioeleweka.

8. Jipe thamani na ongeza thamani kwenye maisha ya mpenzi wako. Kama uko shule soma, kama unafanya kazi fanya vizuri, kama una biashara jitume na kila mara mshauri vizuri mpenzi wako. Hakuna mwanaume anataka kukaa na mwanamke ambaye yupo yupo tu!

9. Acha tabia ya kila saa kuruhusu marafiki zako kuongoza maisha yako. Kuwa na misimamo yako.

10. Kutembea tembea na makundi ya wasichana wenzako kila mahali. Kwani lazima? Huwezi kutembea mwenyewe? Inawezekana kabisa katika kundi la wasichana wenzako yuko ambaye ana tabia za ajabu na mwanaume akimuona tu na wewe atakuhukumu kwa kuwa mko kundi moja. Sio muda wote ni muda wa kutembea na kundi la marafiki.


Kwa Mamen:
​
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]

from bloggers
​
 
Ni hayo tu au kuna mengine umeyaacha?🙄😕😕
 
Aya mkuu! ila la kutoa namba ya simu siioni kama ni tatizo naweza kukupa namba ya simu na vile vile nikakutia kapuni....
 
Kila ndege anatua kwenye mti aupendao....mbona kuna wake za watu wanaishi maisha hayo na waume zao hawajalalamika,ndege wanaofanana huruka pamoja.......ukizoea kulima bustani usitafute mke sinza
 
Mimi bishara za kuhusisa u HOUSE MAID na JUKUMU LA KUWA MKE ndo tunapochefuana mimi na nyie!Kwanini utake nipate unnecessary torture. Mambo ya digitali beki tatu wa kumwaga, mechanisation at its higest niishi kama in the dark 70's aaaaaah wapi!!!!!!!!!!!!

I WILL NEVER MARRY UNTIL I GET A PERSON WHO ENCOURAGES ME TO BE WHO I AM, AND TO FULL FILL MY DREAMS!!!!!!!! PERIOD!!!!!!!!!!! Lakini ndoa where i have to become some one else NOPE!!!!!!!!!!!

Hiyo mi fesibuku,twita, my spesi sijui mautamu yooote ya DOUGLE MASTER 12 wa Instagram wanavochamba watu wima wima mfaidi nyie tu wanaumeeee! Sie tuishi kama 1920's Thubutuuuuuuuuuuuuuu!

Nasisitiza HERI KUWA SPARE TYRE YA LAMBORGIHINI GALLARDO KULIKO TAIRI KUULA GUTA/BAJAJI/BODA
 
mwamamme wa kweli hasifiwi kuweka thread mmu. anasifiwa kwa cash flow yake
 
makavu kwa wanaume wenye maneno bila vitendo. eti umekula? tuma mpesa bhana
 
Kila ndege anatua kwenye mti aupendao....mbona kuna wake za watu wanaishi maisha hayo na waume zao hawajalalamika,ndege wanaofanana huruka pamoja.......ukizoea kulima bustani usitafute mke sinza

hiii nayo ni makavu live shost......
 
Mimi bishara za kuhusisa u
HOUSE MAID na JUKUMU LA KUWA MKE ndo tunapochefuana mimi na nyie!Kwanini
utake nipate unnecessary torture. Mambo ya digitali beki tatu wa
kumwaga, mechanisation at its higest niishi kama in the dark 70's
aaaaaah wapi!!!!!!!!!!!!

I WILL NEVER MARRY UNTIL I GET A PERSON WHO ENCOURAGES ME TO BE WHO I
AM, AND TO FULL FILL MY DREAMS!!!!!!!! PERIOD!!!!!!!!!!! Lakini ndoa
where i have to become some one else NOPE!!!!!!!!!!!

Hiyo mi fesibuku,twita, my spesi sijui mautamu yooote ya DOUGLE MASTER
12 wa Instagram wanavochamba watu wima wima mfaidi nyie tu wanaumeeee!
Sie tuishi kama 1920's Thubutuuuuuuuuuuuuuu!

Nasisitiza HERI KUWA SPARE TYRE YA LAMBORGIHINI GALLARDO KULIKO TAIRI
KUULA GUTA/BAJAJI/BODA

Devil is a liar! mmmmh lara 1
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom