KERO Makato ya Mkopo kwenye Mshahara wangu yananitesa sana. Nilikopa Milioni 10 ili nifanye biashara ya madini ila haijafanikiwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni ajira mpya mwezi wa 10 Halmashauri ya Mbogwe, nilikopa kupitia ESS mkopo wa Shilingi Milioni 10 kwa miaka 8 kufanyia biashara ya madini bahati mbaya nimefeli.

Kinachoniumiza kwa sasa ninapokea mshahara kidogo baada ya makato nawaza hiyo miaka 8 nitaishi vipi?

Ninatembea naongea peke yangu kama kichaa sasa sielewi hata nifanye nini, nikiwashirikisha ofisini ninajua wataanza kunisema badala ya kunishauri.

Natamani kuwauliza watumishi wa umma hii hali inatatuliwa vipi?
 
Mtumishi wa umma anakosa muda wa kusimamia biashara kiasi kwamba akirisk kama alivyorisk mleta uzi ishu isipotiki lazima aone amekosea.

Sasa mkuu let's face it, utaishi maisha magumu huu mwaka wa kwanza. Sijajua Halmashauri yenu mkopo wa Hazina unakuja lini lakini hakikisha huo haukopi, ukikopa iwe ni kwaajili ya biashara za hapo kwa hapo. Mfano kilimo cha nyanya au uuzaji wa simu ama za mkopo au hata siyo za mkopo.

Sijui idara yako kama ni idara yenye safari ongea na senior mpe uhalisia na kama alikua anajimilikIsha safari zote mpe ukweli kwamba hizo safari pia awe anakuconsider.

Kama wewe ni mwalimu. Hiyo aya ya pili iangalie sana na ignore aya ya tatu
 
Tulia uilambe dawa.
 
Uko vzr mkuu.
Tatizo chama lako tu
 
Ulikua unafanya nini exactly kwenye sekta ya madini? Unachimba, dealer/broker, unauza vitendea kazi au?

Japo mtu inabidi uanzie mahali ulipo ila hata 100M ni hela ndogo kuanza nayo kwenye hii sekta.
 
Back
Top Bottom