Makato ya mishahara yaniua

sir ronga

Member
Nov 25, 2016
90
107
Salaam wana JF,

Ni jamaayangu ambaye ni mtumishi wa umma. Ali share na mimi yanayomsibu. Ushauri zaidi unahitajika tafadhali

Namnukuu kwa ufupi;

''Basic salary yangu January 2016 ilikuwa 937,840/=
Ukiondoa makato yote pamoja na mkopo wa bodi, take home ilikuwa 650,900/=
Nikaona July bajeti mpya mishahara itapanda kidogo japo hata 80 hivyo nikajiongeza kuchukua kamkopo nipate japo kakitalu. Nikawa nabakiwa na 410,300/=. Kwakuwa nilikuwa natimiza majukumu yangu kisawasawa serikalini ndani ya siku3 za kazi, siku mbili nilizitumia kujiongezea kipato
Ghafla bin vuu, mambo yakawa tight.
  • Hakuna cha posho wala motisha.
  • Chai na lunch ofisini navyo vikayeyuka (kila mtu ajitegemee. Ni maagizo kutoka juu)
  • Ni lazima kuripoti ofisini kila siku na muda wa kuondoka una saini
Nikajifariji kuwa mwezi wa saba walau kutakuwa na ahueni. Mara hakuna cha nyongeza.
Akili ikavurugika. Ile nawaza pakutorokea, Bodi wakaja na 15%. Nikaomba uhamisho nikimbilie sehemu ambapo nawezakufanya issue nyingine zakujiongezea kipato walau weekend. Wakati nasubiria majibu ya uhamisho, nikasikia uhamisho umepigwa marufuku.
Take home kwasasa nitabakiwa na 335,400/= Hapo sijagusa hata senti.

Ee Mungu,...kama maamuzi ninayotaka kuyafanya kama ni kwa mapenzi yako na iwe hivyo..ila kama siyo kwa mapenzi yako, niepushie kikombe hiki mie mja wako''

Mwisho wa kunukuu. Nilichomshauri nikwamba rudi kijijini ukalime au ukafuge. Mshukuru Mungu hujaoa wala huna mtoto
 
Na mimi naomba umfikishie ushauri wangu, ambao ni huu:-

Wala asirudi Kijijini sababu ameshakuwa mwenyeji hapo alipo.

Cha kufanya ajitahidi sana kujibana kwenye Matumizi, na pia ajitahidi kudunduliza na kujiwekea Akiba. Baada ya Miezi michache atakuwa na kiasi fulani ambacho kitakuwa Jembe la kuanzia miradi midogo midogo huku akiwa anaendelea Kazini kama kawaida.

Baada ya muda mabadiliko atayaona na Jembe litazidi kuongezeka huku yeye akiendelea na Maisha ya kujibanabana, mpaka pale mambo yatakapokaa sawa.

Na kama itawezekana Jembe litakapoongezeka uwezo wa kubadilisha miradi, biashara, inawezekana.

Kwahiyo asikate tamaa.

Muhimu azingatie
 
Mshukuru Mungu hata wewe unatoa hesabu za pesa yako au income yako hapa sasa na huyo ambaye hata hajui kesho pesa ataipata wapi unataka asemeje.

Watz tunalalamika sana kila kitu ni kulalamika tu kwani hiyo kazi umelazimishwa kufanya.

Kama ni makato kwa majibu wa sheria utakatwa tu mpaka sheria itakapofutwa au kurekebishwa hakuna pa kukwepa.
 
Hivi laki 3 mtu mzima anaishije nayo mjini? Watu wanakopa na kuanzisha miradi, huyo jamaa yako yeye anakopa na kununua kiwanja!!!! Somo la ujasiriamali lingefundishwa tokea chekechea tz tungekuwa na millionaires wakutosha
 
Kuna wanaotamani wapate ajira wapokee hata take home ya laki mbili. Chezea magu wewe. Anabana matumizi uku anajenga hekalu kwake.
 
Wewe umekopa ukanunua kiwanja,tena mpitimbi halafu unakuja kulialia hapa JF. Watanzania tunahitaji maombi ya lazima.
 
Maamuzi yako sahii, nakuombea safari yenye mafanikio huko kijijini
 
Mpe pole sana huyu jamaa yako( ambae ni wewe). Hali imekua ngumu sana kuna walim nawafaham wenye ngazi ya mshahara Tgts D1 walikopa nmb wanakatwa kama laki mbili so loan bod wakichukua 15% vijana hawa watakua wakipokea kama 230,000 yani mwal wa diploma atakua na maisha mazuri kuliko wa degree only in tz. 2020 walimu msirudie kosa mmeshajifunza
 
Mpe mchanganuo HARUFU hiyo 315,000 iliyo iliyobaki hebu msaidie kuandika bajeti ya mwezi na atakayosave
Nikianza kwa kugawa ina maana kwa siku anatakiwa asizidishe 10,000 pamoja na kusave
 
Akili ndogo ndilo tatizo kubwa hapo na si makato,Hiyo laki 3.5 mlipe Muha aliyetoka Kigoma kuja Dar kwa miezi 3 tu utaona atavyoizungush ktk biashara ndani ya miaka 3 utamwamkia mbona.Mimi si Muha na nalipwa mshahara wa kima cha chini baada ya kuficha vyeti ili tu niajiriwe serikalini,sijamaliza hata miaka 2 sasa nina kiwanja Dar,duka. Wala sijawahi pata safari au semina ya malipo tangu nianze kazi
 
Akili ndogo ndilo tatizo kubwa hapo na si makato,Hiyo laki 3.5 mlipe Muha aliyetoka Kigoma kuja Dar kwa miezi 3 tu utaona atavyoizungush ktk biashara ndani ya miaka 3 utamwamkia mbona.Mimi si Muha na nalipwa mshahara wa kima cha chini baada ya kuficha vyeti ili tu niajiriwe serikalini,sijamaliza hata miaka 2 sasa nina kiwanja Dar,duka. Wala sijawahi pata safari au semina ya malipo tangu nianze kazi
 
Hivi laki 3 mtu mzima anaishije nayo mjini? Watu wanakopa na kuanzisha miradi, huyo jamaa yako yeye anakopa na kununua kiwanja!!!! Somo la ujasiriamali lingefundishwa tokea chekechea tz tungekuwa na millionaires wakutosha
Laki tatu hela ya bia.

Halafu utasikia kuna MTU anazuia waalimu wasiendeshe bodaboda!!
 
Mkuu usikate tamaa, kila jaribu lina mlango wa kutokea. Badili mtindo wa maisha uendane na hali uliyonayo.
 
Mpe pole sana huyu jamaa yako( ambae ni wewe). Hali imekua ngumu sana kuna walim nawafaham wenye ngazi ya mshahara Tgts D1 walikopa nmb wanakatwa kama laki mbili so loan bod wakichukua 15% vijana hawa watakua wakipokea kama 230,000 yani mwal wa diploma atakua na maisha mazuri kuliko wa degree only in tz. 2020 walimu msirudie kosa mmeshajifunza
ni kweli mim ni dipnoma take home mia saba 20 sina mkopo
 
Ulitakiwa uwe na angalau kitu kinakuingizia kidogo kwa mshaara huo duh tarehe 5 huna kitu utaishia kukopa kwa riba mpaka mkopo uishe
 
Salaam wana JF,

Ni jamaayangu ambaye ni mtumishi wa umma. Ali share na mimi yanayomsibu. Ushauri zaidi unahitajika tafadhali

Namnukuu kwa ufupi;

''Basic salary yangu January 2016 ilikuwa 937,840/=
Ukiondoa makato yote pamoja na mkopo wa bodi, take home ilikuwa 650,900/=
Nikaona July bajeti mpya mishahara itapanda kidogo japo hata 80 hivyo nikajiongeza kuchukua kamkopo nipate japo kakitalu. Nikawa nabakiwa na 410,300/=. Kwakuwa nilikuwa natimiza majukumu yangu kisawasawa serikalini ndani ya siku3 za kazi, siku mbili nilizitumia kujiongezea kipato
Ghafla bin vuu, mambo yakawa tight.
  • Hakuna cha posho wala motisha.
  • Chai na lunch ofisini navyo vikayeyuka (kila mtu ajitegemee. Ni maagizo kutoka juu)
  • Ni lazima kuripoti ofisini kila siku na muda wa kuondoka una saini
Nikajifariji kuwa mwezi wa saba walau kutakuwa na ahueni. Mara hakuna cha nyongeza.
Akili ikavurugika. Ile nawaza pakutorokea, Bodi wakaja na 15%. Nikaomba uhamisho nikimbilie sehemu ambapo nawezakufanya issue nyingine zakujiongezea kipato walau weekend. Wakati nasubiria majibu ya uhamisho, nikasikia uhamisho umepigwa marufuku.
Take home kwasasa nitabakiwa na 335,400/= Hapo sijagusa hata senti.

Ee Mungu,...kama maamuzi ninayotaka kuyafanya kama ni kwa mapenzi yako na iwe hivyo..ila kama siyo kwa mapenzi yako, niepushie kikombe hiki mie mja wako''

Mwisho wa kunukuu. Nilichomshauri nikwamba rudi kijijini ukalime au ukafuge. Mshukuru Mungu hujaoa wala huna mtoto
Laki 3 kubwa Sana, serikali hainabudi kuongeza kodi ubakie na laki 1 tuu inakutosha
 
Back
Top Bottom