Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Mimi ni mteja wa NMB Bank. Katika kurahisisha huduma zangu za kibenki, nimejiunga na huduma ya NMB Mobile Banking. Huwa nafanya miamala yangu kutoka na kwenda benki yangu. Juzi, nilitaka kufanya muamala wa kutoa pesa benki kupeleka kwenye tigopesa.
Kila nikijaribu kuingia kwenye menu ya NMB Mobile sifanikiwi. Sikuwa najua tatizo na hivyo sikufanikisha muamala wangu. Mambo yangu niliyotaka kuyafanya yakakwama. Niliamua kumshirikisha mwenzangu mwenye huduma kama yangu. Yeye ndiye aliyenifumbua macho.
Akaniambia na mimi nikathibitisha kuwa kama huna salio la vocha kwenye simu yako basi huwezi kuingia kwenye menu ya NMB Mobile. Nikaambiwa na kuthibitisha kuwa kila unapoingia menu hiyo, vocha hukatwa. Kumbe, muamala wangu haukufanikiwa kwakuwa sikuwa na vocha!
Kuna makato kwenye vocha na fedha inayotumwa. Makato na tozo kulia na kushoto. Nimeambiwa (bado sijathibitisha) kuwa hata kuingia kwenye menu ya tigopesa kunahitaji uwepo wa vocha simuni ili nayo ikatwe. Tozo na makato yamefika pabaya, yanayafanya maisha yetu kuwa magumu zaidi.
Wahusika fanyeni hima mrekebishe hali hii. It is too much!