Billy ocean (Leslie Sebastian Charles) ni m Trinidad mu English anayeimba nyimbo miondoko ya R&B kimataifa, alitamba sana miaka ya 80. Alikuwa akiimba na pia mtunzi wa nyimbo katikati ya miaka ya 80. Alizaliwa Januari 21, 1950 (Ana miaka 66) huko Trinidad and Tobago. Aliingia kwenye Uk top 20, Ikiwemo na namba 3 kali za marekani. Mwaka 1985 alipata tuzo ya grammy kwa kuwa mwanamuziki bora wa kiume wa miondoko ya R&B na mwaka 1987 alichaguliwa kupewa tuzo ya Brit kwa kuwa mwanamuziki bora wa kiume Uingereza, pia alipata tuzo nyingine nyingi kutokana na umahiri wake katika kutunga nyimbo zake mwenyewe. Ni mshiriki wa imani za ki Rastafari. Alitamba sana na kibao chake maarufu kinachoitwa CARRIBEAN QUEEN ( NO MORE LOVE ON THE RUN) Wimbo huu aliuandika mwenyewe na ulishika namba 1 katika Billboard hot 100 na Black singles chart huko marekani, na namba 6 katika UK single chart mwaka 1984. Wimbo huo ulimpatia tuzo ya akiwa ni mwanamuziki pekee wa Uingereza kupata tuzo hiyo.