Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 19,296
- 68,376
Leo katika Historia:
1965 - Rais wa Marekani Lyndon B. Johnson anatoa amri ya kuongeza idadi ya askari wake katika vita ya Vietnam kutoka 75,000 mpaka 125,000.
Pamoja na yote hayo, Marekani ilishindwa vibaya sana vita hiyo ambayo ilipigwa kwenye misitu minene huko Vietnam.
Leo katika Historia:
1984 - Michuano ya Olimpiki ya majira ya kiangazi yafunguliwa rasmi huko Los Angeles Marekani.
Leo katika Historia:
1993 - Nchi ya Andorra yajiunga rasmi kwenye Umoja wa Mataifa.
Leo katika Historia:
2001 - Ian Thorpe mwanamichezo toka nchini Australia anakuwa muogeleaji wa kwanza katika historia ya michezo hiyo kushinda medali sita za dhahabu katika michuano ya Dunia ya Kuogelea.
Leo katika Historia:
1938 - Albert Fujimori anazaliwa.
Alikuwa Rais wa Peru.
Leo katika Historia:
1954 - Hugo Chavez anazaliwa.
Alikuwa ni kanali katika Jeshi na baadaye kuja kuwa Rais wa nchi ya Venezuela.
Komredi Chavez anakumbukwa sana kwa misimamo yake na isiyoyumba dhidi ya Marekani.
Ni moja kati ya Makomredi walioisumbua sana CIA kando ya Komredi Fidel Castro.
Alifariki mwaka 2013, wengi wanashuku kifo chake kilitokana na faulo toka kwa Marekani.
Leo katika Historia:
1971 - Abu Bakr Al Baghdadi anazaliwa.
Ni kiongozi wa kundi hatari la Kigaidi la Islamic State. ( ISIS )
Yap..Kumbe walikuwa hawatambuliki kabisa[emoji15] [emoji15]
Duuh...ingenyesha feri sijui ingekuwaje?Dunia nayo ina mwembwe huko Thailand nako ilinyeshaga mvua ya samaki
Leo katika Historia:
1981 - Michael Carrick anazaliwa.
Ni kiungo wa Man Utd. Moja kati ya wapiga pasi hodari wa Kiingereza.
Ahsante sana. Uwe na siku njema.View attachment 372256
Mpaka hapo basi sina la ziada asubuhi ya Leo, shukrani kwa kuwa pamoja nami, bila kusahau kuwa magazeti haya yameletwa kwenu kwa hisani ya fix za Bitoz
Sasa nampisha Mussolin5 aje na historia
Muwe na siku njema
KweliLeo katika Historia:
1914 - Austria- Hungary yatangaza vita dhidi ya Serbia.
Hii ilisababisha kuelekea kwa kuanza kwa vita kuu ya kwanza ya Dunia.
Leo katika Historia:
1985 - Mathieu Debuchy anazaliwa.
Ni beki wa kulia wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa.
Hapo sasa,bitoz umemkosha kabisaLeo katika Historia:
1981 - Michael Carrick anazaliwa.
Ni kiungo wa Man Utd. Moja kati ya wapiga pasi hodari wa Kiingereza.