Makapuku Forum

Visa na Mikasa:

Tutakuwa tunaangazia visa na mikasa vilivyowahi kutokea Duniani japo kwa ufupi.

Leo tunaanza na Mkasa wa Samuel K. Doe

Alizaliwa huko May 6 mwaka 1951 na kufariki 1990 huko Liberia.

Alikuwa ni koplo wa Jeshi la Liberia ambapo alimpindua Rais wa nchi yake William Tolbert na kuchukua madaraka na kujipa Urais wa nchi hiyo mwaka 1980.

Alimuua Rais na kumkatakata viwiliwili kisha kumtembeza kwenye mitaa ya Monrovia, Liberia.

Baada ya kuingia tu madarakani akafanya ziara yake ya kwanza nchini Marekani na hivyo kuzua maswali kuwa mapinduzi aliyoyafanya yalibarikiwa na Marekani.

Alitumika na Marekani katika vita baridi, pia katka utawala wake alibadilisha umri ili agombe Urais kwa kuwa katiba ilikuwa haimruhusu. Alitawala kwa mkono wa chuma ambapo Wapinzani wake zaidi ya 50 waliuwawa katika utawala wake.

Alitawala kwa miaka 10, kuanzia mwaka 1980 mpaka 1990, ambapo alipinduliwa katika mapinduzi yaliyoongozwa na Charles Taylor wa Ivory coast ambapo alikamatwa na kuanza kuchinjwa kiungo kimoja baada ya kingine kama masikio, vidole huku akiwa bado mzima kama alivyofanya kwa Rais wake. Baada ya hapo mwili wake ulitembezwa mitaa mbalimbali ya Monrovia. Huo ndio ukawa mwisho wa Samuel Doe nchini Liberia. Ambapo aliingia madarakani kwa upanga na akondoloewa kwa upanga pia.

Kwa leo dawati la Visa na Mikasa halina la ziada. Bitoz tunategemea picha toka kwako.

Tukutane next time!!
 

Kitu poa
Picha za mauaji suweki kuna watu zinawatishaga

..............
 
Safi sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…