Makapuku Forum

Apumzike kwa amani mzee Swalehe.
Huwa nakua na masikitiko makubwa naposikia habari kama hizi, tunaweza kuona kawaida lakini vile umaskini ulivyo mkubwa kwenye jamii yetu familia yoyote inakutana na situation kama hii wanakuwa kwenye wakati mgumu sana na ukosefu wa tumaini na kuchukia maisha kwa ujumla.

Nadhani ile sera ya bima ya afya kwa wote matukio kama haya ndio umuhimu wake ungeonekana.
 
Kweli kabisa
 
Winga wa Kimataifa wa Ghana aliyekuwa anacheza Hatayspor ya Uturuki Christian Atsu mwili wake umepatikana katika kifusi akiwa amefariki kufuatia tetemeko lililotokea nchini Uturuki.

Atsu alikuwa anatafutwa na Timu ya uokoaji kwa muda mrefu na baadaye kudaiwa amepatikana kabla ya Wakala wake Murat Uzunmehmet kuthibitisha kuwa sio yeye aliyedaiwa kuokolewa.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni siku 11 zimepita toka kutokee kwa tetemeko hilo lililoathiri Uturuki na Syria, Atsu amefariki akiwa na umri wa miaka 31 na amewahi kuvichezea vilabu vya Chelsea, Evertona na Newcastle.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewafukuza kazi Askari wake sita katika kipindi cha miezi sita, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu yasiyoendana na maadili ya Jeshi hilo.

Akiongea na Vyombo vya Habari bila kuwataja majina Askari hao, RPC wa Arusha Justine Masejo amesema Askari hao walifukuzwa kazi katika kipindi hicho baada ya uchunguzi wa kijeshi kukamilika kutokana na makosa yaliyokuwa yakiwakabili.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Kivukoni imeahirisha shauri la kikatiba la Uraia pacha hadi Mei 2,2023 ambapo pia yatajadiliwa mapingamizi ya Serikali juu ya shauri hilo ambalo lilifunguliwa December 2022 na Raia sita wa Canada, Marekani na Uingereza wenye asili ya Tanzania.

Kuahirishwa kwa kesi hiyo namba 18 ya mwaka 2022 ni kutokana na Mwenyekiti wa Jopo la Majaji watatu, Jaji Mustafa Ismail kuwa na majukumu mengine ya kiofisi ambapo hata hivyo leo upande wa Jamhuri umewasilisha takribani mapingamizi matatu ukipinga mchakato wa kufunguliwa kwa shauri hilo.

Nje ya viunga vya Mahakama, Wakili wa Wanadiaspora hao Peter Kibatala amezungumza yafuatayo “Shauri limeahirishwa hadi Mei 2 2023 ili kujadili mapingamizi matatu ya kisheria ambayo yameletwa na Serikali wakipinga kesi, kesi kama hizi haziwezi kupita bila mapingamizi hivyo ni mchakato wa kawaida, wamejibu wenzetu hoja za hawa Diaspora pamoja na hoja zao pia wameweka mapingamizi ya mchakato wa kisheria".

Kesi hiyo imefunguliwa na Shaban Fundi, Patrick Nyelesa Nhigula, Restuta Kelemera, Njole Muya, Emmanuel Emmanuel na Bashir Kassam dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo wanaiomba Mahakama itamke kuwa vifungu vya sheria ya Uraia vinavyozuia Uraia pacha ni batili wakidai kuwa vinakiuka haki zao za kikatiba kwa kuwa vinawanyang'anya haki ya asili isiyonyang'anyika kwa maana ya Uraia wa kuzaliwa.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linawashikilia Wafanyakazi wa TRA, Upendo Msigwa mwenye umri wa miaka 32 Mkazi wa Mawelewele na Chali Chaliga mwenye umri wa miaka 28 Mkazi wa Donbosco kwa kosa la kutoa leseni bila kufuata sheria na taratibu za Nchi zinavyotaka.

Akiongea na Waandishi wa Habari wa Iringa, RPC wa Iringa, Allan Bukumbi amesema Wafanyakazi hao wa TRA wamefanya kazi kinyume na sheria hivyo Jeshi la Polisi linawashikilia na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.

Kamanda Bukumbi amesema Jeshi la Polisi liliwakamata Omary Kibao (38), Johnson Kihongosi (31), Dickson Nelson(32) kukutwa na leseni za udereva 31, vitambulisho vya NIDA na Mpiga kura 04, nakala za magari ya Watu mbalimbali na Police loss report.

Aidha Kamanda Bukumbi amesema kuwa Watuhumiwa hao walikuwatwa na namba za magari na Pikipiki 431, TIN numbers 08, printer 05, laptop 1 na desktop 1, nakala za vyeti vya mafunzo ya udereva 02, scaner 01 na lamination mashine 1.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa ushirikiano na Askari wa Uhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa Ruaha wamefanikiwa kumkamata Madambo Nyambinga miaka 27 baada ya kukutwa na silaha moja aina Gobore iliyotengenezwa kienyeji ikiwa imehifadhiwa ndani ya gogo pori la Liyangoro lililopo Kijiji cha Idodi na Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani upelelezi ukikamilika.
 
Shauri jipya la kikatiba linalohusu Uraia pacha lililofunguliwa na Raia sita wa Marekani, Uingereza na Canada wenye asili ya Tanzania ambao ni Shaban Fundi, Patrick Nyelesa Nhigula, Restuta Kelemera, Njole Muya, Emmanuel Emmanuel na Bashir Kassam, leo February 20 2023 limetajwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Kivukoni.

Shauri hilo namba 18 la mwaka 2022 lilifunguliwa December 16,2022 na Raia hao dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia Wakili wao Peter Kibatala ambapo Raia hao waliondoka nchini na kwenda ughaibuni kwa nyakati tofauti hasa katika Nchi za Marekani, Uingereza na Canada ambako wanaishi na kufanya kazi huko baada ya kupata Uraia wa Nchi hizo.

Katika shauri hilo Raia hao wanaiomba Mahakama itamke kuwa vifungu vya sheria ya Uraia vinavyozuia Uraia pacha ni batili huku wakidai kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki zao za kikatiba kwa kuwa vinawanyang'anya haki ya asili isiyonyang'anyika kwa maana ya Uraia wa kuzaliwa ambapo vifungu vyenyewe ni kifungu cha 7(1) na (2) (c), (4) (a) (6) vya sheria ya Uraia.

Raia hawa pia kupitia kiapo chao Mahakamani wamedai kuwa wanaathirika na kitendo cha kunyimwa haki mbalimbali katika Nchi yao waliyozaliwa kwa kuzingatia kwamba walipata uraia wa Nchi hizo kwa sababu tu za kutafuta maisha lakini mapenzi yao kwa Nchi walimozaliwa yako palepale.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…