Makapuku Forum

Mtu mmoja anatafutwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya baada ya kuotesha bangi ndani ya nyumba yake kwenye sebule na kwenye vyumba vya kulala katika eneo la Eldolet mjini Kesese.

Bangi hiyo yenye uzito wa kilo 33.5 ikiwa na thamani ya zaidi ya Ksh 1 Milioni sawa na Tsh. milioni 19.7 imekamatwa nyumbani kwa Mtuhumiwa huyo na baadae ikagundulika kuwa amekuwa akitumia kifaa maalum kinachotumia mwanga wa jua ili kuufanya mmea huo kustawi vizuri na kwa ubora mkubwa.

"Polisi walipewa taarifa na Raia wema kuhusu nyumba hii, Polisi hawakumkuta nyumbani kwake lakini mimea 21 ilipatikana sebuleni, chumbani mimea 68, kwa dinning 14 na kwenye nyumba nyingine jirani na hiyo tukapata mimea 26, Mtuhumiwa hajakamatwa bado mpaka sasa" ——— Polisi wamesema.
 
Peter Moris ( 33 ) fundi ujenzi Mkazi wa Mlole anashikiliwa na Polisi Kigoma kwa kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya Watu saba yaliyotokea katika Kijiji cha Kiganza Mkoani Kigoma huku sababu zikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kamishina wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi Tanzania, Lebaratus Sabas amethibitisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa huyo baada ya siku tatu za upelelezi juu ya tukio hilo lililotokea usiku wa kumkia July 3,2022.

Katika mahojiano na Polisi Mtuhumiwa Peter Moris anadai kumtuhumu January Mussa ambaye nae amefariki katika tukio kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mke wake na hivyo kupelekea kutenda tukio hilo.

Majina ya Watu waliofariki ni Tilifera Toyi ( 70), January Mussa (34) Sara Dunia(28), Joel Mussa (40), Christina Razalo (9), James Joel (7) na James January (3).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…