[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Jana yule Bishoo Bruno Fernandes kila akitaka kushika mipira ya faulo kupiga, Mwanaume Cristiano Ronaldo anamwambia "tulia mdogo wangu hizi shughuli za kiume" [emoji1]
Nachokiona huyu Mtoto Bruno anapaswa sasa kutulia atapata presha kubwa kukimbizana na kivuli cha Ronaldo, hizi faulo na penati naona ni wazi Mnyama ameshapewa sasa
Game dume kama hizi ambazo dunia imechukua upande wake basi anakuwepo Cristiano Ronaldo anakuja kukupa utofauti mkubwa na jana aliitengenisha mechi
Namkumbuka Ronaldo dhidi ya Wolfsburg akiwa pale Real Madrid zile chuma tatu alizoweka ilikuwa ni comeback, aliweka tena tatu dhidi ya Atletico tena nusu fainali ya UEFA hiyo, huyo amezaliwa kwa ajili ya mitihani migumu
Jana dakika za mwisho ametenganisha tena maji na mafuta[emoji119] ni muda sasa wa Bruno kuelewa nguvu ya Ronaldo, yani Ronaldo kafunga moja na Bruno kapiga assists mbili, ila kwenye Mchezaji bora wa mechi, Ronaldo kashinda kwa 41% ya kura dhidi ya wachezaji 16
Ronaldo back to the theater of dreams and dreaming again, Manchester United wana timu mbili! Kwanza United na pili ni Ronaldo