[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Juzi kwenye mchezo kati ya Inter Milan na Lazio kulikuwa na tukio Kati ya Joaquin Correa wa Inter Milan na Luiz Felipe wa Lazio
Baada ya dakika 90 za mchezo ambapo Lazio alishinda 3-1, Luiz Felipe alitoka mbio na kwenda kumrukia Rafiki yake Correa ambaye sasa yupo Inter Milan
Kumbuka kuwa Correa msimu uliopita alikuwa Lazio ila msimu huu amehamia Inter Milan, kumbuka pia wawili hao ni Marafiki wakubwa sana
Luiz Felipe alichotaka ni kumtania Rafiki yake baada ya hayo matokeo ya mwisho! Ila Correa aligeuka kwa hasira na kupelekea ugomvi Mkubwa sana uwanjani na Felipe akapewa kadi Nyekundu
Felipe alilia sana baada ya kupewa kadi nyekundu hiyo tena kutokana na tukio alilomfanyia Rafiki yake Kipenzi ila akamgeuka na kujifanya hamfahamu na akapewa kadi
Felipe alilia sana kwakuwa Correa ni Rafiki yake mzuri na walicheza wote msimu uliopita Lazio, familia zao yani watoto na Wake zao ni Marafiki wakubwa sana
Felipe analia kwakuwa timu zimetenganisha picha yao kubwa na nzuri waliyonayo nje ya mpira, analia sana kwakuwa anahisi Rafiki yake amemsaliti mbele ya Refa na amepewa kadi nyekundu
“Ni Rafiki yangu mzuri ambaye mpira wa miguu umenipatia, ila sina cha kusema zaidi ya kuomba radhi “ kauli ya Luiz Felipe
Kuna la kujifunza hapa! Hakuna Rafiki wa kudumu wala hakuna adui wa kudumu Bali kuna maslahi ya kudumu pekee! Rafiki anaweza kuwa nyoka pia[emoji120]