[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Siku kadhaa nyuma takribani mwezi na nusu niliandika kitu kuhusu UMUHIMU WA NETWORK haswa nikiigusia klabu ya Simba
Network nikasema zipo nne! FEEDER CLUB vs BIG CLUBS, CLUBS VS AGENCIES, CLUBS VS MEDIA na CLUBS vs FEDERATION, Nikatoa Maelezo yangu na kuliacha lipite
Kutokana na changamoto za COVID 19 hivi sasa kumekuwa na idadi maalum ya Mashabiki kuingia viwanjani hii ikiwa inasimamiwa na CAF wenyewe! Ila inatofautiana kati ya klabu na klabu
Simba imetoka taarifa kuwa mechi yao wanaruhusiwa Mashabiki 15,000 kwenye dimba la Mkapa, Biashara ni mashabiki 5,000 pale pale kwa Mkapa na Azam ni 2,000 pekee
Nikatweet kitu kukumbusha post yangu ya miezi nyuma kuhusu NETWORKING! Haswa kwenye CLUB VS FEDERATIONS, yani Klabu na Shirikisho eidha ni TFF au CAF Ila mahusiano yenu Yanaleta tija kubwa kwenye jambo lolote
Nikutumia mfano wa msemo mwepesi sana unasema “The corporate world works differently from the streets” kifupi taasisi zinaendesha mambo yao tofauti na watu wa mtaani wajuavyo, bila mahusiano mazuri ni kuteseka ni lazma ujenge mahusiano
Tanzania Leo hii amepata mkopo kutoka IMF simply ni Network, Ahly anafanya vizuri ukiachana na uwekezaji basi ni Network nzuri na Mashirikisho, hivyo ndivyo taasisi hufanya Kazi duniani
Rais wa CAF Patrick Motsepe ni Rafiki wa karibu na Mwekezaji wa Simba, Rais wa CAF ile klabu yake ni Marafiki wa karibu na Simba, Rais wa CAF ni Rafiki wa karibu na CEO wa Simba, Klabu ya Simba ni marafiki wa karibu na CAF mpaka kuwatambua kwenye SUPERLEAGUE, hizi ni networks
Ulaya hao Real Madrid, Manchester United na miamba mingi mpaka ikasemekana wanapendelewa na UEFA ikazuka HEATED BALLS SCANDAL, Lakini ni watu tu kutojua kuwa Network nzuri inaleta matokeo chanya
Nitaomba takwimu ya timu inayoingiza Mashabiki wengi zaidi ya Simba ukanda huu wa CECAFA kwa ruksa ya CAF, nitaomba takwimu Kama kuna klabu au timu ya taifa imeingiza Mashabiki wengi kwa ruksa ya CAF hivi karibuni zaidi ya hii ya SIMBA
The corporate world works differently from the streets