[emoji3578][emoji3578][emoji3578] Farha Jr
KOCHA THIERRY HITIMANA, BINADAMU BORA NJE YA UWANJA
Jioni moja baada ya Ligi kuu bara kusimama kupisha mechi za kimaitaifa hizi zinazochezwa sasa! Nikipokea simu ya 'wanangu' wanaocheza Ligi Kuu niwasindikize kwenye recovery
Ilikuwa waende swimming kwenye hotel moja hapa Jijini Dar Es Salaam, ofcourse tukaongozana kwenye gari ya Mchezaji mmoja! Wachezaji wapo watatu wa Ligi kuu na Mimi wanne msela tu
Wakati 'Wanangu' hao watatu wameanza kuogelea Mimi sijazoea hayo mambo nikawa nimetulia nachezea simu, walioga kwa muda kidogo ghafla nikaitwa na Mtu nisiemfahamu
Alikuwa ni Mzungu yule tukasalimiana kwa Kiingereza kisha akaniambia wale uliofika nao ni wachezaji mpira kama sikosei! Nikajibu Ndio! Akaniambia wameoga muda mrefu sana waambie yatosha, kwa afya ya misuli kutokana na temperature ya maji
Niliporudi eneo la pool sikuwaambia kuna Mtu kasema inatosha bali nikawaambia, Wanangu tuwahini muda umeenda mimi nawahi kuandaa kipindi basi tukakubaliana tukawa tunatoka nje
Wakati tunatoka bado nikawa nazoom sura ya yule Mzee, nikahisi kama nimewahi kumuona sehemu kwenye mpira wa miguu nilihisi ni Kocha moja wapo wa Simba ila sikuwa na uhakika sana, nikaamua kupotezea
Sasa tulipofika mapokezi ghafla tunakutana na Kocha wa Simba, Thierry Hitimana akiwa ameketi anatazama mechi ya Namungo vs Kagera iliyokuwa inapigwa Ilulu mkoani Lindi
Wale wachezaji wote watatu ambao ni Wanangu wakaenda kumsalimia Mwalimu, kumbuka ni wachezaji wa timu tatu tofauti dhidi ya Kocha wa timu tofauti, Mwalimu anawafahamu vyema wakasalimiana
Nikarudi nyuma kidogo kumuuliza Mhudumu wa pale kuwa Kocha huyo anaishi pale? Akaniambia ndio bench la ufundi lote la Simba linaishi hotelini hapo, nikaunga ile picha ya nyuma kuwa ni kweli yule wa mwanzo alikuwa Kocha wa Simba pia (yule Mzungu)
Sasa Kocha Hitimana kuna sehemu alikuwa anataka kwenda lakini hapafahamu.... ITAENDELEA