
TUOMBE
Baba katika Jina la Yesu Kristo Asante kwa siku mpya ya leo JUMAMOSI JUNE 2 2018 ambayo umetuchagua tena tuweze kuuona Utukufu wako.
Watu wengi walitamani nafasi hii hawajaweza kuiona siku ya leo.
Karibu Roho Mtakatifu shusha Mapaji tuwe Imara .
BABA Tunakuomba Utusamehe makosa yetu yote ambayo tumetenda kwa mawazo kwa maneno kwa matendo na kutotimiza wajibu wetu mbalimbali.
Uturehemu twakusihi.
Tunaomba utusaidie kuwasamehe wale wote waliotukosea Mfalme wa Amani walioomba msamaha na wale ambao hawajaomba msamaha tuwasamehe na kuyasahau yote waliyotutendea
Wabariki wote katika Ndoa zetu na nyua zetu familia zetu Waume Wake Watoto Wasaidizi wa ndani Ndugu Jamaa Marafiki Wachumba wakutafute wewe kwa bidii.
Bariki viongozi wa Serikali wakutafute kwa Bidii Nchi iwe na Amani wakatende haki na kuwa na hofu yako Baba.
Baba Ponya Wagonjwa na ponya dawa wanazotumia zipate kuponya kila jeraha na Ugonjwa na wote wanaouguza waweze kutoa huduma kwa Upendo na wasipungukiwe chochote.
Asante kwa uponyaji wa wagonjwa wote tunaomba Baba uponyaji wa mwili na Roho uwe wa kudumu.
Tunawaombea wajawazito wote na wanaojifungua Baba tunaomba ulinzi wako uwazingire wajifungue salama pia watoto watakaozaliwa wawe salama maana Baba kazi hii ya uumbaji umeianzisha wewe kwao tunaomba iwe ya kukupendeza .
Baba Bariki wasafiri na vyombo Majini Nchi Kavu na Angani ukawe Dereva mwema Damu ya Yesu itufunike tuendako na tunakotoka siku ya leo zuia hatari na ajali zote Mfalme wa Amani.
Baba wafariji Wafiwa Wajane Wagane Yatima Wafungwa Mahabusu Wenye huzuni na wahitaji wote Walioachwa Waliotelekezwa wasio na chakula Waliodhulumiwa wakuangalie na kukutegemea wewe tu.
Epusha Wivu Visasi Masengenyo Chuki Dharau Kiburi Kujisahau na Majivuno ili Sadaka zetu Zikakubalike mbele yako ziwe za Kukupendeza Mfalme wa Amani
Bariki kila kazi za mikono yetu ziwe Halali na za kukupendeza daima.
Baba Asante kwa Sababu Unatupenda na utajibu sawasawa na mapenzi yako.
Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Mpatanishi na Mwokozi wetu Amen
JUMAMOSI NJEMA YENYE BARAKA
DAMU YA YESU ITUFUNIKE

