Makapuku Forum

Huwa ninapenda miziki fulani hivi ambayo huwa inaniondolea sifa yangu ya kuwa kijana na kuniweka kuwa mzee kijana. Nasema hivi kwa nini, kuna hawa wanamuziki wawili. Frank Sinatra na BB King walifariki tarehe kama ya leo miaka tofauti

BB King alifariki 2015, ni gitaa na ushairi wake ndo ulinifanya nimpende na kuupenda muziki wake



Frank Sinatra- huyu ana asili ya Uitaliano, ni maarufu kwa wale watu wa zamani lakini kama mpenzi wa muziki, Sinatra utampenda, alikuwa ni kipenzi cha wadada wa enzi hizo.
Hapa anaimba na Armstrong, unataka muziki gani mwingine tena wa Blues kama hutawasikiliza nguli hawa!




Oh, kabla sijamaliza, leo kazaliwa mjasiriamali na mmiliki wa Facebook, alizaliwa mwaka 1984. Wakati mwingine unaweza kujiuliza kuchagua elimu/kukaa madarasani ndo umaskini wako

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…