Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Tule Pamoja, Furaha Hununuliwa

Moja kati ya mjadala (debate) maarufu kabisa shuleni hasa sekondari na hata kwenye maisha ya kila siku ni ule usemao, 'Pesa Hainunui Furaha' mashabiki na wapinzani hapa walikuwa wanakutana na kila mmoja kusema anavyoona na kutetea upande wake. Ilikuwa ni mjadala mzuri na wa kuvutia iwe unajadiliwa kwa Kiswahili au kiingereza. Upande wa waliosema pesa hainunui furaha ulionekana kushinda mara nyingi lakini haikuzuia wote waliodhani pesa hununua furaha kuondoka na furaha kwamba maoni yao yamesikilizwa. Tafasiri Unavyoweza.

Nikukaribishe tu kwenye tafakari yenye uzoefu wa kibinafsi na hapa ninaweka wazi maslahi yangu kwenye kusema kuwa pesa hununua furaha ni suala la tafasiri tu kugomba na ndiyo maana kipengele hiki kipo. Kwanini ninasema pesa inanunua furaha, sababu ni moja tu, kila mmoja wetu anapenda kuishi kwa furaha na furaha ya pesa haimaanishi kuwa na utajiri wa kupita jirani yako, la hasha. Unaweza kuwa na hela ya mboga na kahawa tu huku mfukoni ukiwa na sarafu kama albaki.

Pesa hununua furaha pale tu utakapoweza kumkaribisha jirani yako na kutumia pamoja, mfano unaweza kuwa na shilingi elfu kumi na ukaona uitumie kwa kununua kitabu cha kujifunza kusoma na ukakipeleka shuleni. amini kabisa kuwa pesa yako imenunua furaha kwa watoto wengi ambao hawana uwezo wa kununua kitabu hicho. Ukimkaribisha rafiki, ndugu au yeyyote uliyekutana naye na ukamlipia nauli ndani ya gari basi umenunua furaha si kwako tu bali na kwa yule uliyemfanyia wema. Atabaki na tabasamu na moyo wako utakuwa na furaha hata wakati unaenda kulala. Tafasiri unavyoweza
 
Muziki: Two In One

.....two in one usifikiri naongelea ule wimbo mzuri wa taarab ya Alhaj Mzee Yusuf, la, hapa namaanisha naunganisha salamu za kukuuliza kuhusu weekend yako ilivyokuwa na kukutakia wiki njema. Upande wangu mambo yalikuwa mazuri sana, nashukuru sana kwa kuendelea kuwa hapa na kulifanya Jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo.

Wiki ya kazi ndo imeanza na kati ya miezi mirefu sana mojawapo ni huu, huwa una wiki tano, sijataka uhesabu kisha ukazikosa unaanza kuniuliza mbona kwaresma imeangukia mwezi huu na easter itakuwa lini, endelea kufunga na kama hujafunga kama anko wangu Lyon Lee basi angalau funga mlango unapoingia chooni sio kukaa unajikoholeshakoholesha kama umeshikwa na chemba moyo.

Nikushukuru sana Nyagei mtaasisi kwa kuliweka hai Jukwaa kwa wikend yote na ninarudia tena kutoa taarifa kuwa tangu mwaka umeanza weekends zote hata nikiwepo jukwaani siwezki muziki. Muziki ni siku za kazi tu maana natumia bundle la ofisi.

Muziki sasa, two in one inahusisha kipengele cha muziki na ombi la mtaasisi mwenzangu Nyagei ambaye ametaka tuburudike na wimbo huu toka kwa mrembo mkongwe le madame Mbilia Bell

 
Ahsante sana mtaasisi kwa kutupia good music from Mbilia Bell
 
Bado natafakari mtaasisi, huku naburudika na muziki mzuri toka kwa mwanamama fundi Mbilia Bell,



Hivi Mbilia Bell ana undugu na Alexander bell?
 
Bado natafakari mtaasisi, huku naburudika na muziki mzuri toka kwa mwanamama fundi Mbilia Bell,



Hivi Mbilia Bell ana undugu na Alexander bell?

Ha hahhahahhaa, Mbilia Bell na Alexander Bell waliishi karne tofauti kabisa, nchi tofauti kabisa na mmoja Alexander alivumbua simu na mawasiliano ya simu tunayoyafurahia sasa huyu mwingine dada yetu alikuwa akiumiza kichwa kutunga nyimbo nzuri tunazofurahia leo
 
Tafasiri Unavyoweza: Hakuna Jipya, Amua La Manufaa

....ukweli usemwe, kuna wakati watawala wetu wanatutengenezea matatizo, wanajidai kuyaongelea ili tuwaone wanajali. Hili si tatizo lao, ni la kwako wewe na mimi ambao tunakaa na kuwasikiliza wakiongelea na kujidai wanayafahamu matatizo yetu. Fikiria na jipe muda wa kuangalia mambo na ikiwezekana jaribu kubadili watawala, itakusaidia na watakuheshimu ukiwapa madaraka, tafasiri unavyoweza
 
Lakini watakuwa wana gene's same hawa viumbe wawili [emoji124] [emoji124]
 
Tafasiri Unavyoweza: Taarifa Sahihi

Unaweza kufanya maamuzi sahihi si kwa sababu tu una nguvu na utashi, hivi vyote havitoshi kufanya maamuzi sahihi kama hujajua udhaifu wako katika kufanya maamuzi sahihi. Kwa maana hiyo basi, unahitaji si kujua nguvu na udhaifu wako tu katika kufanya maamuzi sahihi, unahitaji zaidi ya hivi vitu viwili vya msingi. Na hivi vitu vya msingi vinakuwa ni nguvu au udhaifu pale tu unapokuwa na taarifa sahihi. Tafasiri unavyoweza.

Usione wadau wanapigania uhuru wa habari (ikihusisha kupata, kusambaza taarifa) na uhuru wa maoni katika taifa. taarifa sahihi ni nguvu, ukikosa taarifa sahihi uwezo wako wa kufanya maamuzi sahihi unakuwa mdogo sana yaani inakuwa ni kama unapoamua kufanya maamuzi ukiwa umelewa, hasira au furaha iliyozidi kipimo. Mara zote ukifanya maamuzi katika hali hizi baadaye uwezekano wa kujutia ulichofanya ni mkubwa zaidi. Tafasiri unavyoweza, wakati wa uchaguzi watu wanaopiga kura kwa kipande cha kanga, sabuni na chumvi huku kesho yake wakilia kuhusu ukosefu wa ajira, maji na huduma nyingi za kijamii.

Tafuta taarifa sahihi ili ufanye maamuzi sahihi, utakuwa na nguvu ukiwa na taarifa na kaa ukijua kabisa kati ya umaskini mkubwa kwa jamii yetu ni ukosefu wa taarifa. tafasiri unavyoweza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…