Tafasiri Unavyoweza: Kundi Letu, Maoni Yetu
Maoni ya kundi yana nguvu, huwa hayaji hivi hivi tu au kwa bahati mbaya. Huja baada ya mazungumzo na mijadala mipana ambayo wakati mwingine kabla hujasikia hitimisho unaweza kudhani kundi husika hataelewana. Kwa taarifa yako tu ni kuwa, kundi ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye malengo waliyokubaliana. Bila malengo basi kundi linabaki kuwa mkusanyiko wa watu.
Kwanini ninaandika haya ili wewe utafasiri unavyoweza, kumekuwa na dhana tofauti kuhusu Makapuku Forum, kundi hili limekuwa, bora sasa, likishambuliwa bila ya washambulizi kuchukua japo nafasi kidogo ya kulifahamu. Kiuhalisia kulianzishwa hadi nyuzi kadhaa kuwa kundi hili uzi wake ufutwe na wengine walipoona umoja unaooneshwa na Makapuku waliamini Makapuku inapaswa kuwa Jukwaa linalojitegemea. Tafasiri Unavyoweza.
Siku zote, kama unataka kujua maana ya kitu basi jipe nfasi ya kutokuwa na upande, itakusaidia kujua zaidi na hapo ndipo utaweza kuwa na nafasi ya kuchagua upande. Ukiwa na maoni yako tayari, kutafuta maoni ya mwingine ni kupoteza muda. Humu ndani tumo watu wa kila namna, kada, na jinsi. Tunatofautiana kwa mwengi sana na tunajijua kuwa tunatofautiana lakini siku zote tofauti zetu ndiyo umoja wetu.
Mijadala ya makapuku kama kikundi huwa haiwi rahisi, hujadiliwa na majadiliano aidha ya siasa, uchumi, falsafa, muziki, utamaduni au maisha ya kila siku huwa sio rahisi. Na kwa ugumu huo, majadiliano huzaa hitimisho na kuelewana au kukubaliana kutoelewana (our discussions as a group enhance majority opinion). Watu hujadiliana, hutofautiana na hukubaliana kutofautiana lakini mara nyingi Makapuku forum katika JF ni kama hadithi ndani ya hadithi. Tafasiri Unavyoweza