Muziki: Nguvu ya Dhaifu
Kama kuna makosa ambayo yalikuwa na faida ni kwa wengi kuwadharau wachache, wakiwaona kuwa wachache ni dhaifu kuzidi wengi na hivyo wengi watafanya wanavyotaka. Mnyonge kanyimwa nguvu ya kukupiga tu ila misuli ya mdomo wake haichoki kusema kuwa unahitaji kupunguza ubabe wako na kumsikiliza mnyonge. Ninakusalimia sana kapuku mheshimika, nafurahi kukuona hapa na zaidi wewe
Slim5 ,
Yeth lottah (hivi wewe kama unaweza kubet mbona sikukuona kwenye forex, joke),
Malcom Lumumba karibuni sana wadau, hapa ni sehemu nzuri mkiwepo.
Nguvu ya mnyonge huishi miaka mingi maana huwa haishii kusema tu kwa mdomo, huandika pa na maandishi yanaishi siku zote. Unakumbuka kwenye zama za kutaka kuwepo kwa vyama vingi nchini, wengi waliwakataa wachache/wanyonge lakini kumbe wengi walifanya maamuzi wakiwa wamenyong'onya (lazy thinking). Matokeo tuliyaona, wachache wape na ndo tunaishi na demokrasia ya wachache, wengi wanafuata na kubadilika itachukua muda.
Muziki sasa, anko wangu kwa sasa ni kama kachanganyikiwa yaani kule kanda ya kaskazini alikoenda amejikuta anakumbuka utamu alioucha kwa aunt yangu, yaani kachanganyikiwa, anarudi kwa aunt yangu, nimefurahi na nyie endeleeni kumuombea, atubu.