Makapuku Forum

Ahahahhah binamu wewe ila mbona nasikia chanjo yako ipo lakini ipo juu sana
 
Muziki: Utambulisho

...eeeh, kaa (sio mdudu, au kuweka makalio chini) ukijua kabisa kuwa kuna tofauti ya utambulisho hauhusiani na ugeni au kutojulikana. Suala la msingi ni wewe unataka utambulishweje, wengine tunawajua na tunawatambua kwa namna walivyo na tukichoka kuwatambulisha tunawawekea na lebo kama zile za bei, wanauzwa. Najiaminisha kwako wewe kapuku mheshimika kuwa wewe unajitambua kama Kapuku na kaa ukijua ukapuku sio ule tunaoufasiri mitaani, sisi ni zaidi ya hao na ndo maana tuko humu tukiwa na kila na aina ya ukapuku wa utajiri. Utaitafuta maana siku nyingine kwa wakati wako.

Sijaingia hapa kutambulisha mtu au kitu ila nimeingia hapa nikiwa na nia moja tu ya kukuchangamotisha (challenge +motivation) kuwa ni vizuri kujitambua kabla hujatambulishwa. Ukifanyiwa utambulisho, anayekutambulisha anaweza akakosea asikuseme wewe, kama ilivyotokea kwa anko wangu pale alipomruhusu mume wa mjumbe amtambulishe, kumbuka huyu muwe alikuwa na bifu ya kuchukuliwa mke na anko wangu sasa utambulisho ukawa ni kuvuana nguo wakati anko alikuwa kapiga suti kama diwani mpya.
Muziki sasa, jitambue binafsi na wengine wote tutakutambua bila kukuwekea kitambulisho, kama wewe ni mwalimu basi kuwa mwalimu kweli, kama ni askari fanya yanayostahili kufanywa, na ukiwa mkulima basi baki kuwa mkulima na sio mshamba. Na kama wewe unafanya mazuri ongeza, ukiwa unafanya mabaya, zidisha lakini kaa ukijua hutakiwi kutambulishwa na mwingine wakati una uwezo wa kujitambulisha mwenyewe. Nakupenda Kapuku na unalijua hilo.

 
Dj Obe Asante
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…