Makapuku Forum

Makapuku Forum

9cbef8593ed11c0e742b89f63c592ca5.jpg
 
Asante sana BlessedHope kwa maneno ya baraka, asante anko Lyon Lee kwa UF na asante kwetu sote tulio hapa. Magazeti yatawajia muda si mrefu (itapendeza zaidi ukijua kwamba mimi huwa siweki magazeti, subirini shululu aagane kikubwa na Tumosa ndo atayaleta).

Tukumbuke tu kifungua kinywa unaweza amua hata kula kiporo, sio kila morning chai na chapati mbili.





...
 
Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kwa Upendo wako,fadhili zako na kutuamsha tukiwa wazima na Afya njema,wapo watu wengi walitamani kuiona siku ya leo Baba hawajaweza ,tunatoa Sifa ,Shukurani,Heshima na Utukufu kwa Neema hii.

Tunakuja Mbele zako tukikukabidhi siku ya leo ya Jumatatu 13 Novemba 2017 ikawe njema na ya kukupendeza.
Tunaomba toba kwa yote tuliyokosea.Kwa mawazo ,maneno na matendo na kutotimiza wajibu wetu mbalimbali Uturehemu twakusihi.
Tuimarishe ili tukupende,
tukuheshimu na kuishi maisha ya kukupendeza wewe tu.
Tunaikabidhi Nchi yetu iwe na Amani.
Tunazikabidhi Familia zetu zidumishe Upendo na Mshikamano.
Tunawakabidhi wagonjwa na wenye shida mbalimbali majumbani na mahospitalini Baba ukawaponye miili na roho pia.
Baba wasafiri wote majini,nchi kavu,angani ukawe nao waende na kurudi salama.Na familia zote Baba mwema zikawe salama na Amani itawale.
Watoto wetu popote walipo makazini,majumbani na mashuleni ukawasimamie wakawe vichwa si mikia wafanye mambo yote kwa ufanisi na mafanikio.Tunaendelea kuwakabidhi watoto wetu wenye mitihani ya masomo mbalimbali onekana kwao Baba,uwepo wako utawale katika mitihani yao na wawe washindi,
Baba Mungu tunazikataa kazi zote za shetani zisipate nafasi katika maisha yetu tunazivunja kazi zote hizo katika jina la Yesu Kristo tunamwaga damu ya Yesu Kristo ikatakase kila pando na kuling'oa na kulitupa kuzimu Mfalme wa Amani.
Tunakabidhi kazi zote za mikono yetu zikapate kibali mbele yako nawale wasio na kazi na shughuli za kufanya Baba wape kazi ,waliofanya usaili mahali popote takasa njia zao waweze kupata kazi baba na maarifa ili wauone Utukufu wako,funguabmilango yote ya baraka Baba mwema..kila tuingiapo na kutoka utubariki.
Baba Asante kwa Matendo yako Makuu yasiyo na mwisho,tunauona ukuu wako siku zote za maisha yetu tunasema Asante Baba na tunaomba uzidi kutuimarisha imani zetu zipande na kuwa viwango vya juu ili tuweze kushuhudia matendo yako siku hadi siku.Roho Mtakatifu tutie nguvutuondoe hofu na mashaka tuliyo nayo.
Nakushukuru maana utatenda yote sawa na mapenzi yako
Katika jina la Yesu Kristo naomba naamini na nashukuru Amen

SIKU NJEMA WAPENDWA MBARIKIWE
Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom