7/Taiwan
Namuona mjomba Side Mnyamwezi anakatiza kitaani na fulana yake kubwa aina ya Form 6 mabega yakiwa juu kwa ndani shingoni nyuma imeandikwa Made In Tauwan
Kuna mtu mzima ambaye hajawahi kuvaa nguo kutoka Taiwani? Inawezekana ushazivaa sana bila kujua kama zimetoka huko
Wataiwan wapo vizuri kwenye uzalishaji nguo tena wamelenga soko la Afrika kama Wachina vile maana huku tunapenda vya bei chee ....buku 1 tu unajibebea !!
Viwanda vya uzalishaji huchangia pato la USD 180 Bilioni ambayo ni sawa na theluthi(1/3) ya GDP ya Taiwani
Gharama za kuwalipa wafanyakazi viwandani ni wastani wa USD 9 tu kwa saa
Viwanda hupigwa kodi ya moja kwa moja ya 17%(corporate tax rate)
......