Makapuku Forum

Makapuku Forum

TETESI ZA USAJILI LEO

795fd95227f1ab2373097cf074a55e44.jpg


a50809a802dee824f5023bd4e89709cb.jpg



Tuanze na waliosajiliwa leo .....

Nathan Ake tokea Chelsea amejiunga na Afc Bournemouth ....
7d49e40efa4a9853dc74ba8399d7e163.jpg



Twende sawa....

Arsenal wamejitoa katika mbio za kumwania nyota wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na sasa wataelekeza nguvu zao kumpata Alexandre Lacazette na Thomas Lemar (Mail Online).
76c25ed3e81c087d2360f8691588225a.jpg


Mesut Ozil ameonesha dalili za kubakia Arsenal baada ya kulipia tena chumba maalum cha kutazamia mpira (executive box) ndani ya uwanja wa Emirates (The Sun).
f7fafef67dc6941015714c17e3d3c99b.jpg


Antonio Conte hajafurahishwa na hatua ya Chelsea kumfuatilia Romelu Lukaku badala ya Andrea Belotti. Conte ameghadhibishwa kwa sababu wachezaji hao wawili bei yao ni moja, takriban pauni milioni 85, lakini mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo ameamua kumfuatilia Lukaku badala ya Belotti (Daily Star).
703147508a989c5b09139e71844f5de4.jpg



Guangzhou Evergrande hawana mpango wowote wa kumuuza Paulinho kwenda Barcelona (Nanfang Daily).

Liverpool wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 70 kumtaka kiungo wa kimataifa wa Guinea Naby Keita, 22 anayeichezea RB Leipzig (Mirror).

Liverpool wanataka kuwasajili Naby Keita pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 23 (Liverpool Echo).

Liverpool wanataka kumsajili beki wa kushoto Andrew Robertson kutoka Hull City (Liverpool Echo).
Real Madrid huenda wakamsajili Eden Hazard, 26, kutoka Chelsea na Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Diario Madrista).
8185030d5be5be53f2bb8aeb61c833d0.jpg


Everton watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Malaga, Sandro, 21, wiki ijayo (Liverpool Echo).

Alvaro Morata amewaambia marafiki wake kuwa ameamua kujiunga na Manchester United na kuwa mkataba tayari “umekamilika” (Daily Express)
62e8fafe6326d6139646110dfe06a57b.jpg


Manchester United hawatomuuza Ander Herera kwenda Barcelona, licha ya taarifa kusema Barca watafikiria kumchukua iwapo watamkosa Marco Verratti, 24, kutoka PSG (Independent)
24a94ba0c7dda73dec588e067cd5781d.jpg


Barcelona wanamtaka Ander Herera na Riyad Mahrez, kama watashindwa kumsajili Marco Verratti (Sport.es).

Radja Nainggolan anayesakwa na Manchester United, huenda akajiunga na Inter Milan, baada ya klabu hiyo ya Italia kutoa dau la euro milioni 60 (101 Great Goals).

Jose Mourinho anafikiria kumchukua kiungo wa Middlesbrough Marten de Roon katika wiki chache zijazo (TuttoMercatoWeb).

Manchester City wameanza mazungumzo na Tottenham kuhusiana na beki wa kulia Kyle Walker, lakini Spurs hawataki kupokea chochote chini ya pauni milioni 50 (The Mirror).

Manchester City huenda wakaamua kumfuatilia winga wa Bayern Munich Kinglesy Coman (RMC).

Chelsea wanafikiria kumfuatilia beki wa Roma, Kostas Minolas, 26, ambaye alikuwa anakaribia kujiunga na Zenith St Petersburg kwa pauni milioni 26 (London Evening Standard).

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anaghadhibishwa na jinsi klabu yake inavyoendesha shughuli za usajili (Star).

Real Madrid bado wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, licha ya klabu hiyo kusema haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo kutoka Ubelgiji (OK Diario).

Chelsea wanajiandaa kutaka kupanda dau kwa beki wa Bayern Munich Jerome Boateng (Daily Mirror).

Chelsea wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa PSG katika kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (The Mirror).

Southampton wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 ambaye thamani yake ni pauni milioni 25 (Sun).

Meneja wa Watfrod Marco Silva amedhamiria kumsajili Kieran Gibbs, 27, kutoka Arsenal. Beki huyo pia amehusishwa na kuhamia Liverpool (Mirror).

Monaco hawatarajii kumuuza Thomas Lemar, 21, msimu huu, na wamewaambia Arsenal na Tottenham kuwa mchezaji huyo hauzwi (Independent).

Licha ya tamko hilo, Barcelona nao wamesema wanamtaka Thomas Lemar (L’Equipe).

Mshamnuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie huenda akarejea katika EPL msimu ujao na kujiunga na Crystal Palace (Daily Mirror).

Meneja mpya wa Nantes, Claudio Ranieri anamtaka kipa wa Arsenal David Ospina (France Football).

Meneja wa Brighton Chris Hughton amethibitisha kuwa klabu yake imewasiliana na Liverpool kuhusu kumsajili beki Joe Gomes, 20 (Brighton Argus).

Beki wa Hull City Andy Robertson, 23, anasakwa na Liverpool, kwa sababu Jurgen Klopp anataka kusajili beki mpya wa kushoto (Liverpool Echo).

Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness amesema hawatomsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka Arsenal, kwa kuwa klabu yake inazingatia kusajili wachezaji chipukizi (Kicker).

Mtoto wa Zinedine Zidane, Enzo, 22, ameondoka Real Madrid na kujiunga na Alves kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu, baada ya kukosa namba katika timu inayofundishwa na baba yake (FourFourTwo)...
c1ba1c38f5942c7c2a19dd9811fd37a4.jpg


Kiungo Saul Niguez, 22, anataka kubakia Atletico Madrid, lakini huku Barcelona na Manchester United zikimtaka, anasema angependa kupata pesa
0fe345584fe34074bfc3473d977fc65e.jpg


Mwenyekiti wa West ham David Gold amesema hawamfuatilii Jack Wilshere, 25, lakini klabu yake inatafuta washambuliaji wawili wapya na wenye uzoefu wa EPL (TalkSport).

Newcastle wanakaribia kumsajili beki wa Eibar, Florian Lejeune, 26, na pia wanataka kumshawishi Andre Gray, 26 kutoka Burnley (Newcastle Chronicle).

5ccfa2e8af8351098a0edb49d18aea4e.jpg



Kesho nayo sikuuu
 
Jielimishe, ijue Darussalaam

KUTANA NA NCHI YA BRUNEI, NCHI YENYE UTAWALA WA KUSTAAJABISHA ZAIDI DUNIANI.

1. Brunei ukipenda iite 'Darusalaam' ama nyumba ya amani ni nchi ambayo raia wake hawalipi kodi YEYOTE. Hata maisha ya wananchi wake ni mazuri na mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa saa (Tshs 50,000), huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa 5% tu.

Serikali inalipa gharama zote muhimu, mpaka chakula kinalipiwa ruzuku. ukifanya kazi kule hakuna income tax (There is no personal income tax or capital gains tax). Sultani anasimamia vizuri sana export ya mafuta na gesi.

GDP ya Brunei imepanda hadi 56% kuwa nchi ya tano duniani (16.11 billion USD in 2013) na IMF wanasema nchi hiyo haidaiwi HATA shilingi MIA.

2. Sultan wa Brunei Mohammad Hassan Bolkiah ndiye Raisi tajiri kuliko maraisi wote duniani, Maarufu kwa utumiaji wa dhahabu kwa kila kitu, hali ila na vijiko vya dhahabu, na nguo anazo vaa zimepambwa kwa dhahabu na fedha. Huyu anamiliki Jumla ya MAGARI 5000 YA KIFAHARI (tazama kasri na moja ya gari lake lake la dhahabu tupu pichani).

Sultan huyu anamiliki pia ndege aina ya Boing 747 thamani yake ikiwa ni dola milion 100 ambamo pia nakshi pekee ni dola milioni 120 humo utakuta vyoo na vyumba vya dhahabu, pia anamiliki ndege ndogo sita na helicopta moja. Arusi ya mtoto wa Sultan wa Brunei ilifanyika kwa muda wa siku 14 kwa gharama ya 5 milion dolla huku watu wote walioalikwa wakila na kunywa na kusaza, na kuhudhuriwa na zaidi ya maraisi 25.

3. Elimu ni Bure kabisa na watoto chini ya miaka 12 HUTIBIWA BURE huku watu wazima wakilipia dola 1 tu kwa Matibabu. Kadhalika ukioa tu unapewa na gari. Ni nchi mojawapo ambayo ina uwiano mkubwa wa watu na magari (1:209)-Ikiwa hakuna tiba ya ugonjwa wako Brunei unapelekwa nje ya nchi hasa Malaysia na Singapore kwa gharama za serikali.

4. Pombe imepigwa marufuku kabisa kisiwani Brunei ingawa wageni wanaweza kuagiza kiwango chenye ukomo na Hakuna NGURUWE hata mmoja nchi nzima.

5. Ukiwa Brunei marufuku kupoint kutumia kidole cha shahada kuonesha kitu. Kidole gumba tu hutumika kupoint kitu na ni Lazima kuvua viatu unapoingia nyumba yeyote ndani ya Brunei.

6. Hii inatumia mfumo wa SHERIA ambapo 'Wezi hukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe'. Mwaka 2014 ilipitisha sheria ya kupigwa kwa mawe hadi kufa yeyote atakayebainika anafanya USHOGA (Homosexual) lakini kwa uthibitisho wa mashahidi WANNE.....Unaweza kusherehekea Noeli (X-mass) lakini si kwa kuweka mapambo yake kama vilemti wa Xmass nk.

7. Ingawa Kisiwa cha Brunei Kina BUNGE lakini nchi hiyo HAINA Uchaguzi, Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 1962, kuna chombo kimoja tu cha habari kinachomilikiwa na Serikali, ni aghalabu sana kwa media kuipinga serikali

8. 93% ya watu wote Wameenda Shule kwa kiwango cha DEGREE.
714a30608d6e9234c283f4fdc3d79d04.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom